MWAKYEMBE APOKEA RIPOTI YA UCHUNGUZI "MADUDU "BANDARI YA DAR ES SALAAM

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, (Kulia), akipokea ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya wizi na madudu mengine kwenye bandari ya Dar es Salaam, kutoka kwa mwenyekiti wa kamati iliyochunguza "madudu" hayo, Bernard Mbakileki, ofisini kwa waziri jijini Dar es Salaam Jumapili Oktoba 21, 2012. Kwa mujibu wa Mbakileki, ripoti hiyo ya kurasa 285, imegundua mambo kadhaa :machafu" na imetoa mapendekezo kadhaa ya hatua za kuchukuliwa ambapo waziri mwenye dhamana amewaahidi watanzania kuwa taarifa ya hatua zitakazochukluliwa kufuatia ripoti hiyo, zitatolewa Desemba mwaka huu wa 2012 ambapo amewataka Watanzania kuvuta subira kwani kuanzia sasa, yeyote anayefanya kazi Bandarini, akithubutu kunyofoa kitu basi nayeye atanyofolewa. Banadari ya Dar es Salaam, imekuwa kwenye shutuma nyingi, ikiwemo kuchelewesha mizigo ya wateja, urasimu lakini baya zaidi wizi uliokithiri wa mizigo ya wateja. Waziri Mwakyembe aliunda kamati hiyo kuchunguza tuhuma hizo kufuatia hatua yake ya kumnsimamisha kazi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari hiyo, Ephraem Mgawe na wasaidizi wake

Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza "madudu" kwenye bandari ya Dar es Salaam, Bernard Mbakileki, akisoma ufupisho wa ripoti yao. Picha zaidi Bofya K-VIS BLOG

Post a Comment

Previous Post Next Post