RAYUU AFUKUZWA KWAO KWA SABABU YA PICHA ZA UTUPU ALIZOPIGA

WAKATI msanii wa bongo movie Rayuu, picha zake zinazoonesha sehemu kubwa ya mwili wake na tattoo kuvunja mtandaoni, ishu hiyo sasa imechukua sura mpya baada ya kudaiwa amefukuzwa kwao na sasa amepata makazi ya muda kwa mkurungezi wake Mr Chuzi ambaye mara nyingi amekuwa akimshauri kuachana na vitendo vinavyoweza kumchafulia jina lake.

Mtandao wa
DarTalk, ulimtafuta Rayuu ili azungumzia ishu ndipo alipodai kuwa wazazi wake walizipata habari zake ndipo waliamua kuchukua hatua hiyo tena bila hata kumpa nafasi kujitetea na kuwaeleza mambo yalivyokuwa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa wazazi wake awali hawakujua habari hiyo lakini kuna baadhi ya watu ambao walikuwa na kinyongo na msanii huyo ndiyo waliopeleka habari hizo pamoja na picha nyumbani kwa madai kuwa wanataka kumkomoa.


Msanii huyo alidai kuwa hakuwa na njisi kwani waliofanyan hivyo ni watu ambao mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi pamoja lakini hajui ni kwanini wamefanya hivyo ingawa hataki kujua sababu kwa sababu anaweza kuchukua hatua nyingine ambayo si nzuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post