SCORPION GIRLS - ATUKUBAKWA NA HATUJAWAHI KUBAKWA


Kundi jipya la Scorpion girls na linalofanya vizuri kwa sasa kwenye bongo fleva linaloundwa na warembo watatu yaani MIRIAM JOLWA a.k.a JINI KABULA, ISABELLA MPANDA a.k.a BELLA a.k.a MRS KALAMA NA RASHIDA WANJALA wamefunguka na kusema tetesi zilizokuwa zikienea kuwa wao walibakwa katika show iliyofanyika sinza sio za kweli na kudai kuwa watu wamewachafua sana na hiyo kesi ambayo ilitokea kwa wasanii wa SNURA ambaye pia anafanya mziki kwa sasa,,,

hata hivyo walizidi kufunguka na kusema kwamba hawataimba nyimbo za mapenzi kwani kila mtu anaimba mapenzi ila wao watajihusisha na wale wanaopenda kuingilia maisha ya watu na kuyaongelea yasiyowahusu na pia wamesisitiza kuwa mbali na hayo pia wataimba nyimbo zitakazohusu maisha halisi ya Tanzania na serikali kwa ujumla

Post a Comment

Previous Post Next Post