Shabiki huyo akimshughulikia kipa Chris Kirkland |
SHABIKI Aaron Cawley - ambaye aliingia uwanjani na kumshambulia mlinda mlango Chris Kirkland, amehukumiwa kifungo jela miezi minne.
Kijana
huyo mwenye umri wa miaka 21, kutoka Cheltenham, alimvamia kipa huyo wa
Sheffield Wednesday katika mechi ya timu yake ya nyumbani, Leeds Ijumaa
usiku na kumshambulia kwa sababu alikuwa anajiangusha kupoteza muda,
timu hizo zikiwa zimefungtana 1-1.
Mwendesha
Mashitaka, Paul Macaulay alisema Cawley aliiambia Polisi alifanya hivyo
kwa sababu alikuwa amelewa na hakumbuki kabisa tukio hilo, ambalo
limeonwa na mamilio waliotazama Televisheni.
Post a Comment