Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa
ndege mjini Quebec, Canada
tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani (IPU)
unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21 Oktoba, 2012 na kumalizika
26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa wabunge wanne kutoka Tanzania,
ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge
kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya
awali ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa
baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127
wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad
Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada Joseph Sokoine akimkabidhi
Mhe. Spika taarifa ya maandalizi ya mkutano huo pamoja na hali ya
kisiasa ilivyo nchini Canada baada ya kuwasili kuhudhuria Mkutano wa 127
wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU).Picha na Owen Mwandumbya-BUNGE
Post a Comment