WASHINDI WA BACLAYS MKOBO BONANZA WAPATIKANA.

  Mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Benki ya Baclays, Samuel Mkuyu(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mshindi wa kwanza wa droo ya promosheni ya ‘Mkopo Bonanza’ ambaye atasamehewa marejesho ya mkopo wake ya miezi kumi na mbili.Droo hiyo iliyochezwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Meneja wa Bidhaa wa benki hiyo, Adam Mbaga na Mkaguzi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha ya Taifa, Majid Bakari.
  Meneja wa bidhaa wa Benki wa Baclays, Adam Mbaga akichagua  karatasi ya mshindi wa kwanza ya droo ya promosheni ya ‘Mkopo Bonanza’ iliyochezeshwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Taifa, Majid Bakari  na Mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Benki ya Baclays, Samuel Mkuyu
Mkuu wa kitengo cha bidhaa wa Benki ya Baclays, Samuel Mkuyu(wa pili kushoto) akisoma jina la mshindi wa kwanza wa droo ya promosheni ya ‘Mkopo Bonanza’ iliyochezwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Taifa, Majid Bakari na ni Meneja wa Bidhaa wa benki hiyo, Adam Mbaga
 
Na Mwandishi Wetu.


BENKI ya Barclays leo hii imehitimisha promosheni yake iliyojulikana kama “Barclays Mkopo Bonanza” kwa kuwapata washindi wa bahati nasibu iliyochezeswa jijini Dar Es Salaam. Bahati nasibu hiyo ilichezeshwa mbele ya waaandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari na ilihudhuriwa pia na mwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha,Majidi Bakari
Akizungumza na waandishi wa habari Bi. Sarah Munema, Meneja Masoko wa benki ya Barclays alisema kwamba benki ya Barclays ilianza rasmi promosheni ya “Barclays Mkopo Bonanza” kuanzia mapema mwezi wa tano mwaka huu. Kampeni hii ililenga kutoa mikopo kwa watu binafsi ambao ni wafanyakazi wa serikali, makampuni na taasisi. Promosheni hii ilitoa kivutio cha kutoa zawadi ya kusamehewa marejesho kwa kipindi fulani kwa wateja wenye bahati watakaochaguliwa baada ya Draw kuchezeshwa mwishoni mwa promosheni hii. Bi Sarah aliendelea kusema, “Promosheni hii ilikuwa na lengo la kuwapatia wateja wa benki yetu nafasi ya kufikia ndoto zao kwa kuwapatia mikopo itakayowapa uwezo wa kifedha wa kufanya yale wanayokusudia. Maelfu ya wateja wetu wamenufaika na “Barclays Mkopo Bonanza” na kama tulivyoahidi, leo hii tuko hapa kwa ajili ya kuchezesha Draw itakayopata washindi watakaosamehewa marejesho ya mikopo yao kwa vipindi maalum”. Alielezea kwamba mshindi wa kwanza atasamehewa marejesho ya mkopo aliopata kwa kipindi cha miezi 12, hii itategemea kiasi cha mkopo aliopata na marejesho aliyopangiwa. Washindi wengine ishirini watajipatia zawadi ya kusamehewa kiasi cha marejesho yao ya mwezi mmoja kila mmoja.
Naye bwana Adam Mbaga, Meneja Bidhaa wa benki ya Barclays alielezea kwamba japokuwa promosheni ya “Barclays Mkopo Bonanza” imemalizika na washindi wa Draw kupatikana, benki bado inaendeleza huduma ya kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, makampuni na taasisi. Aliwahamasisha watu mbalimbali kujitokeza kufungua akaunti na kufaidika na mikopo hii. Mikopo hii inatolewa kwa wafanyakazi katika viwango tofauti hadi kufikia shilingi milioni hamsini kwa mtu mmoja kutegemeana na kiasi cha mshahara wake.
Bi Sarah Munema alimalizia kwa kutoa shukrani za dhati kwa wateja wote wa Barclays Bank kwa kuchagua benki hii. Aliwaomba kujitokeza kwa wingi kutembelea matawi ya benki hii kote Tanzania kufungua account na pia kuomba mikopo kwa ajili ya kujiendeleza katika maisha yao ya kila siku.
Baada ya kuchezeshwa draw ya bahati nasibu, washindi waliobahatika kupata zawadi ya kusamehewa marejesho katika “Barclays Mkopo Bonanza” walikuwa ni;Washindi ishirini waliosamehewa marejesho ya mwezi mmoja ni;Carol Joseph,Jane Hemed,Shaban Bakari,Paulina Gabriel,Abdalah Said,Idd Seleman,Mohamed Athuman,Godliver Wiliam,Godfrey Beba,Zuberi Nungu,Ashura Benedict,Richard Membu,Kulwa Gerge,Moses Joseph,Dastan Jemes,Jane George,Peter Joseph,Obrien Zadose,Hadija Mohamed,Sangalali Michael.
Mshindi wa kwanza aliyesamehewa marejesho ya miezi kumi na mbili ni;Veronza William ambaye ndeye mshindi wa kwanza

Post a Comment

Previous Post Next Post