Mwandishi wa Habari wa Chanal Ten Muniri Zakaria
akiuluza maswali katika Kikao kilichofanywa na Wawakilishi wa CCM kutoa kauli
ya Kulaani machafuko yanayoendelea ambayo yamesababisha kuchomwa Moto Maskani
ya CCM ya Kisonge Mjini Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan CCM
akifafanua jambo katika Kikao kilichofanywa na Wawakilishi wa CCM kutoa kauli
ya Kulaani machafuko yanayoendelea ambayo yamesababisha kuchomwa Moto Maskani
ya CCM ya Kisonge Mjini Zanzibar.
PICHA NA-MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR
Wajumbe wa baraza la wawakilishi (ccm)
wamelaani vikali vitendo vinavyoendelea kufanywa na jumuiya ya mwamsho kwa
kuvunja amani, utulivu na kusababisha vurugu katika mji wa zanzibar kuanzia
jana.
Hapo jana kundi
la mwamsho lilivamia nyumba za watu maduka na kupora bidhaa kadhaa katika
maduka na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza na
waandishi wa habari huko mbweni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi, mhe.
Hamza Hassan Juma kwaniaba ya wawakilishi wa Ccm amesema wakati umefika kwa
serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla hali haijawa mbaya zaidi.kwani
kuendelea kukaa kimya kwa Serikali kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Amesema
serikali imeunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa kasoro zilizokuwepo
na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na usalama na kuweza kuondoa tofauti zao
za kisiasa.
Amesema isifike
pahala Zanzibar ikawa kama zile nchi zenye machafuko na kuwafanya wanachi wake
kushindwa kuishi kwa amani na salama.
Hivyo wajumbe hao
waliitaka serikali mara moja kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika na
ghasia hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Aidha wamemtaka
mkuu wa Jeshi la Polisi IGP na makamanda wenzake kuwajibika moja kwa moja juu
ya suala hili ili kukomesha mambo hayo.
Halkadhalika wajumbe
hao waliitaka serikali kulipa fidia mali zote zilizoharibiwa kutokana na fujo
hizo na kuviruhusu vikosi vya smz vkusaidia katika kuweka ulinzi na
usalama ili maafa zaidi yasije yakatokea.
Akizungumzia
suala la kufutwa jumuiya hiyo, Mhe. Hamza amesema jumuiya ya mwamsho si chama
cha siasa ni jumuiya ya kidini lakini imeonekana kukosa muelekeo na kufanya
vitendo vinavyowafarakanisha waumini wa dini hiyo, kuwagawa. na kuidhalilisha
dini yenyewe ya kiislam.
Hivyo waliitaka
taasisi inayohusika kuifuta Jumuiya hiyo kwa vile inakwenda kinyume na malengo
na dhamira ya kuanzishwa kwake.
Kuhusu kutoweka
kwa Sheikh Farid, Mhe. Hamza amesema hadi hivi sasa haijulikani wapi alipo na
nani aliyeyemchukuwa au kumteka nyara kwa vile kwa mara ya mwisho inasemekana
alikuwa na dereva wake.
Wajumbe hao leo
waligoma kuingia katika baraza wakilaani kitendo hicho na kusema kwamba kesho
watapeleka hoja binafsi kwa spika wa baraza hilo ili kujadiliwa suala mwamsho
na vitendo vyake dhidi ya serikali .
Post a Comment