Mahakama
nchini Misri imewapa hukumu ya kunyongwa watu saba walioshukiwa
kuitengeza filamu iliyosababisha kero na ghadhabu katika ulimwengu wa
kiisilamu mapema mwaka huu.
Maandamano yalifanyika kote duniani kupinga Marekani
Hasira dhidi ya filamu hiyo iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed,
ilisababisha maandamano dhidi ya Marekani kiasi cha kuteketezwa ubalozi
wake nchini Libya.
Washukiwa hao saba walihukumiwa wakiwa hawapo mahakamani.
Hukumu hizo ziliidhinishwa na Mufti mkuu nchini Misri ambaye pia ni msomi wa dini ya kiisilamu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa ni nadra kwa Mufti kupinga hukumu kama hizi.
Filamu hiyo iliyokuwa ya hali ya chini mno, ilitengezwa mjini Carlifonia, Marekani na kutolewa kwenye internet mwezi Septemba.

Miongoni mwa wale walioshtakiwa ni mtengezaji wa filamu yenyewe Morris Sadek ambaye ni raia wa Misri.
Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti
Mahakama itatoa hukumu ya mwisho mwezi Januari kufuatia itikio la Mufti
Post a Comment