
Msanii wa kike wa nchini Kenya, Avril ameamua kuonesha kuwa biashara
ya headphones inaweza kufanywa na msichana pia kwa kuanzisha aina ya
ear/headphones zake ambazo kama zikiwa na ubora mzuri huenda kwenye soko
la Afrika Mashariki zikatoa upinzani kwa zile za Dr Dre Beats By Dre.
Hata hivyo mradi wake huo utapewa shavu na wizara ya elimu ya juu, sayansi na teknolojia ya nchini Kenya.
Ear phones hizo zitajulikana kama Gs N Fs na zitakuwa sehemu ya mradi
wa kuwainua vijana wenye vipaji na mawazo kuhusiana na teknolojia ambao
hawana rasilimali za kuendeleza vipaji vyao.
Post a Comment