![]() |
Safari: Ashley Cole na Frank Lampard (chini) watatemwa Chelsea |
MAGWIJI wa Chelsea, Frank Lampard na
Ashley Cole wataondoka mwishoni mwa msimu baada ya Rafa Benitez
kuthibitisha kubomoka kwa kikosi cha ubingwa cha Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji wote hao wanamaliza mikataba
yao mwishoni mwa msimu na kocha mpya wa Chelsea amesema hawastahili
kuendelea kubaki Stamford Bridge baada ya msimu huu.
Lampard, mfungaji bora namba tatu wa
kihistoria wa Chelsea, ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England,
manne ya FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika miaka yake 11 ndani
ya klabu hiyo.

Cole, aliyejiunga na Chelsea akitokea
Arsenal mwaka 2006, ameshinda taji la Ligi Kuu ya England, manne ya FA
na Ligi ya Mabingwa kwa kipindi chake cha kuishi Stamford Bridge.
Benitez alionekana kwenye picha na
Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo wakiwa kwenye chakula cha usiku na
mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.
"Nilitumia saa kama mbili au tatu na
mmiliki, tulizungumzia kila kitu. Anafahamu mawazo yangu, lakini
hatukuwa na muda wa kutosha pamoja. Labda wakati mwingine tena.
"Kama unajiamini na kujieleza, kila
mmoja anaweza kukuelewa. Mtazamo wangu kwa mmiliki, ni mtu mzuri.
Unaweza kuzungumza naye na ni mwelewa. Anapenda kuona una mawazo mazuri

Mipango ya muda mfupi: Rafa Benitez anataka kuendelea na wachezaji waliopo Chelsea hadi mwisho wa mikataba yao

Si Torres pekee: Benitez anataka kuiboresha timu nzima
Post a Comment