22 Novemba 2012
Klabu
Bilicanas imefika nafasi 10 bora za klabu Afrika Mashariki kwenye shoo
ya Hyped East Africa. Klabu hii, iliwakaribisha Hyped East Africa shoo
ya kwanza Africa inayo tembea Afrika Masharika inayoonyeshwa kwenye Zuku
Pay Tv juu ya Zuku Afrika Channel 100 walifanya pati ya kuvutia kwa
watu waliohudhuria. Alikuwepo John Waititu aka Dj Nijo mwenyeji wa
kipindi cha Hyped East Africa na wenyeji wao Dj Ejay na Paul wa
Bilicanas. Pati hio ilihudhuriwa na vijana wengi kuwakilisha Dar es
Salaam na kuifanya iwepo katika orodha ya klabu bora Afrika Mashariki.
Palipambwa
na ubora wa hali ya juu na watu walipata nafasi ya kupiga picha kwenye
red capeti na walijiskia kama ma supa star. Pia walipata nafasi ya
kujishindia zawadi za Zuku.
Shoo
ya klabu Bilicanas itaonyeshwa Jumamosi ya tarehe 24 Novemba kwenye
Zuku Afrika channel 100 sa 2:30 usiku. Kama hukuudhuria sherehe unaweza
ukafurahia na kuhisi kama ulikewepo pia.
Akizungumza
juu ya ujao Hyped East Africa juu ya shoo ya klabu Bilicanas, Shella
Thiong'o wa Wananchi Programming alisema, "Sisi tulifurahia sana pati ya
klabu Bilicanas na watu walivyokuja kuwakilisha Dar es Salaam.Tulicheza
usiku nzima na klabu ina nafasi nzuri ya kuchaguliwa katika klabu bora
katika Afrika Mashariki ". Aliongeza kuwa, bado wanaendelea kutafuta
klabu bora na wanaelekea safari ya pili Uganda na kurudi Kenya kabla
ya mwisho wa mwaka. Aliendeleza mwaliko kwa watu wote kutembelea Hyped
East Africa katika ukurasa wa Facebook na Twitter na kutuma maoni yao
juu ya pati.
Hype
East Afrika ni kipindi cha kwanza cha burudani kinacho tembea. Shoo
hiyo awali imetembelea Club Sun Cirro na Nyumbani Lounge Dar es Salaam,
Club Anje Noire na Cayenne mjini Kampala na klabu zingine 8 katika miji
mbalimbali nchini Kenya. Hyped Afrika Mashariki inaonyesha juu ya Zuku
Pay TV channel kila Jumamosi saa 8:30.
Zuku
hutoa programu mbalimbali za mitaa maudhui na hurushwa hewani kwenye
chaneli ya Zuku Afrika. Hii ni sehemu ambao kampuni inataka kutoa
burudani kwa mitaa maudhui kutoka kwa wadau wa ndani katika kanda.
Aidha, Kampuni inataka kukua ndani ya sinema sekta kwa kutoa jukwaa la
kimkakati ambayo wadau wote wanaweza kufaidika.
Televisheni
ya Zuku inatoa uchaguzi mpana wa stesheni za burudani ikiwa ni pamoja
na Habari, Michezo na Sinema, majarida na muziki. Hivi vinajumuisha
chaneli za nje kama vile BBC, MTV Base, Sentanta Sports, MGM movies na
zinginezo nyingi. Pia Msambazaji hutoa ofa kabambe za stesheni kama vile
Zuku Afrika ambayo huonesha bara la Afrika, Zuku Maishaambayo huonesha
makala mbalimbali, Zuku Michezo pamoja na chaneli lukuki za sinema.
Huduma hii ya Zuku hupatikana kupitia satelaiti Tanzania nzima.
Post a Comment