
Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, muimbaji aliyewahi kutamba
nchini, Buibui amerejea tena akiwa chini ya uongozi mpya wa Tanzania
Music Power, TMP.
TMP ambayo ni jumuia mpya ya kiharakati iliyoingia rasmi katika
kuokoa kizazi cha muziki wa Bongo fleva Tanzania imeingia makubaliano na
msanii huyo ambaye jina lake ni Frank Lewis Katende Kivunike.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari TMP imesema imeingia
makubaliano na Buibui baada ya kukiona kipaji chake na juhudi zake
katika kufanya kazi ya muziki wa kizazi kipya.
“TANZANIA MUSIC POWER inatambua uwepo wa vyombo vya habari na mchango
wao katika tasnia ya muziki,hivyo inawaomba wasanii, wanahabari na
wadau wote wa muziki kusaidia katika kuwainua wasanii ambao wamechangia
kuuweka muziki wa Tanzania ulipo sasa,” imeandika katika taarifa yake.
“Historia ya Buibui ni ndefu sana toka alipo zaliwa mpaka sasa na
muda si mrefu TANZANIA MUSIC POWER itatoa kitabu cha maisha ya BUIBUI
kuanzia watu aliowahi kushirikiana nao na mpaka kudondoka katika tasnia
ya muziki.
BUIBUI amerudi sasa na T.M.P inatarajia kutambulisha wimbo wake mpya
ambao utaanza kurushwa hewani rasmi baada ya kumalizika kwa makubaliano
ya mwisho na TMP.
Hivyo basi tunapenda kuchukua nafasi hii kuomba watanzania wote
kumpokea BUIBUI,tunatanguliza shukrani za dhati kwa watanzania wote.”
Post a Comment