Wachezaji wa
Burundi, wakimpongeza Chris Nduwarugira baada ya kufunga katika mchezo wa Kundi
B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi
ya Somalia Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. Katika mchezo huo,
Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika
ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84
na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.
|
Post a Comment