Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezaeshaji Kiuchumi, Anaclet Kashuliza akizungumza wakati wa kuzindua shindano la kuandika michanganuo ya biashara litakalo shirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam lililodhaminiwa na Benki ya CRDB.
Amesema
Ujasiriamali ni moja ya jitihada zinazoweza kumletea mtu binafsi,shirika
na hata katika ngazi ya kijamii mabadiliko ya kimaendeleo iwapo fursa
za kibiashara zinazopatikana zitatumika ipasavyo.
Bw.
Kashuliza amesema ili fursa hizo ziweze kutumika kuleta maendeleo
Wajasiriamali wanapaswa kupata elimu ya Ujasiriamali na kuifanyia kazi
kwa vitendo na sio kuishia madarasani.

Ofisa Masoko
wa CRDB, Emmanuel Kiondo akizungumzia malengo ya CRDB kudhamini
Shindano la kuandika mchanganuo wa biashara kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu
katika hafla ya uzinduzi wa shindano la kuandika michanganuo ya
biashara na kuvishirikisha vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam.

Country
Managing Partner wa Ernest & Young Bw. Joseph Sheffu Country
akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa shindano la kuandika
michanganuo ya biashara kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Dar es
Salaam ambapo amesema angependa kuona kadri siku zinavyokwenda tasnia ya
Ujasiriamali inazidi kupanuka ikiwa na wataalamu wa kutosha.

Mkurugenzi
wa Kitivo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDEC), Maria
Nchimbi akitoa nasaha kwa wanafunzi na kuwapongeza shule ya Biashara ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDBS) kwa kuandaa wazo hilo ambalo
limepokelewa vyema na wadau wa biashara na hivyo kufikia kuandaliwa kwa
mashindano hayo.

Afisa
Mahusiano na Mawasiliano wa University Entrepreneurship Challenge 2012
Bw. Dennis Paul akitambulisha Kamati uliyofanikisha uzinduzi wa
mashindano hayo na kutoa wito kwa makampuni na wadau wengine wajitoe
kudhamini mashindano hayo.

Kamati ya maandalizi ya UNIVERSITY ENTREPRENEURSHIP CHALLENGE kutoka shule ya Biashara ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya biashara vya jijini Dar es Salaam.




Mwanafunzi
wa Mwaka wa tatu BCOM Accounting wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Joyce
Wilfred Fungo akielezea marajio yake kujijenga kibiashara pindi
atakapohitimu masomo.

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na uongozi wa UDEC.

Post a Comment