
Mashambulizi yakiendelea
ISRAEL imeshambulia maeneo ya wapiganaji katika
ukanda wa Gaza kwa siku ya tano (Novemba 18, 2012), wakishambulia kwa
ndege na jeshi la majini wakati jeshi lake lingine likijitayarisha
kufanya mashambulizi ya ardhini. Misri hata hivyo inaona ishara za
uwezekano wa kupatikana usitishaji wa mapigano hapo katika siku za
baadaye.
Wapalestina 47, karibu nusu yao wakiwa ni raia, ikiwa ni pamoja na
watoto 12, wameuwawa katika mashambulio hayo ya Israel , maafisa wa
Palestina wamesema. Karibu maroketi 500 yaliyofyatuliwa kutoka Gaza
yamefika nchini Israel, na kuuwa watu watatu na kuwajeruhi wengine
kadha.
Israel ilianzisha mashambulizi yake makubwa ya anga siku ya Jumatano,
na kumuua kiongozi mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, kwa lengo la
kuwazuwia wapiganaji katika eneo hilo la pwani kushambulia kwa maroketi
jamii inayoishi katika eneo lake la kusini mwa nchi hiyo.
Taifa hilo la Kiyahudi limeshambulia hadi sasa kwa makombora 950 kwa
kutumia ndege za kijeshi dhidi ya eneo hilo dogo la pwani la
Wapalestina, wakilenga vifaa vya kijeshi pamoja na kubomoa nyumba za
wapiganaji na makao makuu.
Mashambulio yaliendelea usiku wa manane Jumapili, huku ndege za
kivita zikishambulia maeneo kutoka baharini. Shambulio la anga lililenga
katika jengo mjini Gaza ambalo ni la ofisi za chombo cha habari cha
Kiarabu na kuwajeruhi waandishi watatu wa televisheni ya al Quds, kituo
cha televisheni ambacho Israel inakiona kuwa kinaunga mkono kundi la
Hamas, wamesema watu walioshuhudia.
Mashambulio mengine ya alfajiri dhidi ya nyumba katika kambi ya
wakimbizi ya Jebalya yamesababisha kifo cha mtoto mmoja na kuwajeruhi
watu wengine 12, wamesema maafisa wa hospitali. Mashambulio haya
yanafuatia taarifa za kikaidi zilizotolewa na msemaji wa kijeshi wa
Hamas Abu Ubaida, ambaye amesema katika mkutano na waandishi habari
kuwa, “duru hii ya mapambano haitakuwa ya mwisho dhidi ya maadui wa
kizayuni na ndio kwanza inaanza.”
Shambulio la Israel siku ya Jumamosi limeharibu nyumba ya kamanda wa Hamas karibu na mpaka na Misri.
Israel hata hivyo ikiwa na vifaru na vifaa vingine vya kijeshi imeweka majeshi yake katika mpaka, ikiashiria kuwa bado inafikiria uwezekano wa mashambulio ya ardhini ndani ya Gaza. Baraza la mawaziri la Israel limeamua siku ya Ijumaa, (16.11.2012) kuongeza mara dufu idadi ya wanajeshi wa akiba katika operesheni ya Gaza kufikia 75,000 na wanajeshi wa akiba wanaofikia 16,000 tayari wamekwishaitwa.
Israel hata hivyo ikiwa na vifaru na vifaa vingine vya kijeshi imeweka majeshi yake katika mpaka, ikiashiria kuwa bado inafikiria uwezekano wa mashambulio ya ardhini ndani ya Gaza. Baraza la mawaziri la Israel limeamua siku ya Ijumaa, (16.11.2012) kuongeza mara dufu idadi ya wanajeshi wa akiba katika operesheni ya Gaza kufikia 75,000 na wanajeshi wa akiba wanaofikia 16,000 tayari wamekwishaitwa.
Israel imesema kuwa shule katika eneo lake la kusini zitafugwa leo
Jumapili(19.11.2012) kuepuka madhara zaidi kutokana na mashambulio ya
maroketi ambayo yamefika hadi katika mji mkuu Tel Aviv katika siku
chache zilizopita.
Ndege za Israel zilishambulia Makao Makuu ya Hamas huko Gaza ikiwemo
ofisi ya waziri mkuu baada ya baraza la mawaziri la Israel kuidhinisha
kuandaliwa kwa wanajeshi wa akiba 75,000 kwa uwezekano wa kuvamia Gaza.
Ndege hizo za Israel zimeshambulia wizara ya ulinzi na jengo la ofisi
ya Waziri Mkuu Ismail Haniyeh ambapo hapo Ijumaa alikutana na Waziri
Mkuu wa Misri. Kwa siku kadhaa miripuko mizito imekuwa ikilitingisha
eneo la Gaza linalokaliwa na idadi kubwa ya watu na kusababisha kufuka
kwa moshi mzito angani.
-DW
-DW
Post a Comment