
NINAPO TAMANI KUONA SULUHU YA ZIWA NYASA
Kumekua na
mvutano kati ya Tanzania na Malawi unao sababishwa na mpaka katika Zawa
Nyasa.Historia inaonyesha kuwa mvutano huo ualianza mala tu baada ya Uhuru wa
Malawi mwaka 1964 ambapo wakati huo
ikijulikana kama Nyasaland. Ikumbukwe kwamba Candido Jose da Costa Cardoso
mfanya biashara mkubwa na maarufu wa kireno wakati huo ndie mtu wa kwanza
kufika (kuligundua) Ziwa Nyasa mwaka 1846 kabla ya David Living Stone ambae
alifanikwa kufika mwaka 1859, na baadae Muingereza kuzitawala nchi zinazo
lizinguka Ziwa hilo na kuitwa Nyasaland. Mvutano huo umechukua sura mpya hivi
karibuni baada ya serikali ya Malawi kusema kwamba Ziwa lote ni mali yao, hali hiyo
ilisababisha waziri wa mambo ya nje na ushiriano wa kimataifa wa Tanzania,
Benard Membe kusema Tanzania ipotayari kwa lolote katika kutetea ziwa Nyasa
.Alitoa msimamo huo bugeni wakati akisoma hotuba ya wizara yake tarehe
06/08/2012 (jumatatu)na kuitaka Malawi kufanya mazungumzo na Tanzania,lakini
ikumbukwe kwamba tarehe 04/08/2012, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi,Ephraime
Chiume alisikika akisema kwamba, kwa mujibu wa mkataba wa mwaka 1890(Heligoland
Teaty) ambao ulisainiwa kati ya Uingereza na Ujerumani unawapa malawi umiliki
wa Ziwa hilo, alisisitiza kwamba hata Maazimio ya Umoja wa Afrika yanatambua
ziwa hilo ni lao.
Tanzania
ilipata habari kupitia shirika la TPDC (Shirika la Taifa la maendeleo ya
petrol)kua eneo lote la Ziwa Nyasa,kaskazini mwa Msumbiji limegawanywa kwenye
vitalu,na kwamba serikali ya Malawi imetoa vitalu hivyo kwa kampuni ya utafiti
wa mafuta na gesi,Serikali ilikua na ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti
zenye uwezo wakutua majini na ufukweni zinazokadiriwa kua tano zilionekana
zikivinjari katika eneo la Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kati ya January 29 na
Julai 2,mwaka huu(mwaka 2012)licha ya kunyimwa kibali na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania. Hali hiyo ilisababisha serikali ya Tanzania kuitaka
Malawi kutoruhusu mtu au kampuni yoyote ile kuendelea na shughuli za utafiti
kwenye eneo lote linalobishaniwa, serakali ya Tanzania iliamua kuimalisha
ulinza katika Ziwa Nyasa hali ambayo ilisababisha hofu kwa Malawi wakijua
kwamba mapigano yatatokea baada ya ulinzi unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uchokozi kutoka
Malawi.
CHAZO CHA MVUTANO KATI YA TANZANIA NA MALAWI
Baada ya uhuru
wa Malawi mwaka 1964 serikali ya nchi hiyo imekua ikidai na kuamini kwamba
mpaka wetu na wao kwenye Ziwa Nyasa unapita pwani na kwa maana hiyo Ziwa lote
la Nyasa kutoka kwenye mpaka wa msumbiji( Mozambique) hadi Malawa ni mali
yao.wanadai kwamba mkataba uliowekwa saini kati ya waingereza na wajerumani
mwaka 1890 uliweka mpaka kwenye pwani au ufukwe wa Ziwa Nyasa mkataba huo
unajulikana kama Heligoland treaty or Anglo- German Agreement.
Kwa upande wa
Tanzania, tunadai kwamba mpaka kati yetu na Malawi kwa Ziwa Nyasa unapita
katikati ya Ziwa hilo,kutoka pale Malawi na Msumbiji (Mozambique) wanapopakana,
usawa wa Nyuzi 11 Kusini hadi mwisho wa Ziwa kule Kyela kwenye digrii 9 kati ya
Ziwa, kwa madai kwamba Nyaraka na ramani zilizo tengenezwa na wakoloni wetu
mwaka 1928,1937 na mwaka 1939 zinaonyesha kuwa mpaka wa Ziwa hilo upo katikati.
Mwaka 1967
kulikua na vita kali ya maneno ( A serious war of words) kati yetu na Malawi,
hali iliyo sababisha mpaka kushikishana adamu kidogo katika maji ya Ziwa Nyasa
baina yetu na Malawi kutokana na uhusiana mbaya uliokuwepo wakati huo kati ya
Rais Julius Nyerere na Hastings Kamuzu Banda wa Malawi wakati huo, hii ni
kutokana na Rais Hastings Kamuzu Banda Kuunga mkono Serikali ya kikaburu nchini
South Africa ambayo mwalimu Nyerere alikua haungi mkono.
TANZANIA IZINGATIE YAFUATAYO KATIKA MZOZO HUU
Tuwe wamoja katika kupambana na Malawi, serikali lazima
ihakikishe kwamba wa Tanzania wote tunakua wamoja katika kipindi hiki cha mzozo
wa Ziwa Nyasa, huu si wakati wakuleta mpasuko wa kisiasa, ikumbukwe kwamba
Rais wa Malwai Joyce Banda amesha kutana
na viongozi wa vyama vya upinzani akiwataka kuwa wamoja katika kupigania nchi
yao. Hivyo basi wa Tanzania lazima tutambue kwamba katika mgogoro huu
tunazidisha umoja ili tuweze kuisaidia serikali yetu, niombe serikali ikutane
na wadau tofauti katika kuhakikisha tunajipanga kuikabili Malawi.
Tusi idharau Malawi, Serikali na
Watanzania kwa ujumla wetu hatupaswi kuitazama Malawi kama nchi dhaifu na isiyo
weza kufanya jambo lolote kwetu, adui
dhaifu anaweza akafanya maajabu na kuishagaza dunia( We don’t need to
underestimate our enemy). Lazima tutambue kwamba katika mzozo kama huu adui nae
anatafuta mbinu za kutushinda, hivyo basi lazima tujipange kwa lolote litakalo
tokea lakini tusidharau Malawi.Lazima
tujue wana hoja gani na sisi tunahoja gani halafu tunapigana vipi, tuache
propaganda zisizo na msingi katika kulindi maslahi ya nchi yetu nasio kuwaona
Malawi kama wadhaifu wasio na mipango na nguvu katika kupigania Ziwa
Nyasa.Tujiulize nguvu ya chokochoko hizi zimetoka wapi? Kama wao ni dhaifu vipi
wame kuwa manunda katika hili,hivyo basi laziwe tuwe wakali katika kutetea Ziwa
Nyasa bila ya kuona Malawi kama nchi dhaifu.
Tukumbuke mzozo wa Kagera,watanzania
lazima tukumbuke vita vya kagera mwaka 1978 hadi 1979 pamoja na chuki, uadui na
uhasama kati ya Mwalimu Nyerere na Iddi Ammin Dada, baada ya Uganda kudai
kwamba mpaka wa nchi hizi mbili ni mto kagera na kusababisha kuvamiwa kwa
kaskazini magharibu( Bukoba) mawa Tanzania Octoba 30,1978 na kutekwa kwa eneo
kubwa la nchi yetu hali ambayo ilitughalimu kulikomboa. Hivyo basi hatakama tuna
nguvu ya kuipiga Malawi kivita hatu paswi kukimbilia katika suala hilo kwani
tukikurupuka itatu gharimu kama ilivyo kuwa kwa Iddi Ammin Dada.Licha ya Iddi
Ammin Dada kuondolewa Novemba 25,1978 na April 11, 1979 adui kuikimbia Uganda
lakini Tanzania ilidhohofika sana, kwa mfano uchumi wetu ulizorota na kuyumba
vibaya sana pamoja na ulemavu wa kudumu ambao wazalendo waliokuwa wakikomboa
nchi yetu waliupata. Je tumejipanga na kufikiria haya kabla ya kusema Tanzania
ipo tayari kwa lolote?
Tukusanye ushahidi wa kutosha ilituwe na
vielelezo thabiti vya kuishinda Malawi, Serikali lazima ipitie nyaraka
muhumu kwa kufanya uchambuzi makini( cross-examination) wa nyaraka mbalimbali
mbazo zipo, tusiwe wepesi wa kufanya maamuzi bila ya kuwa na uthibitisho katika
mambo nyeti kama haya( A delicate diplomatic matters of the state). Tuwe na
uthibitisho sahihi kwa kusoma nyaraka zote , zile zinazo semekana ni za kweli
na zile zinazo lalamikiwa kutokakna na mapungufu ili tujilidhishe na tuwe wenye
kujiamini tunapo tetea Ziwa Nyasa letu.
Malawi ni kibaraka wa nchi za kigeni,
Watanzania kuna kila sababu ya kukubali na kuamini kwamba Rais Joyce Banda na
serikali yake ni vibaraka wa nchi za kigeni hivyo basi hata katika mzozo wa
ziwa nyasa inawezekana akawa anasukumwa na nchi hizo, kwa mfano serikali ya
Malawi imekubaki ndoa ya jinsia moja ili kuendana na matakwa ya wahisani wa
kigeni kama uingereza kwa kisingizio kwamba misaada kutoka uingereza itasaidia
kutatua tatizo la umasikini. Swali ni je
serikali gani duniani ambayo inaweza kujikwamua na umasikini kwa kutegemea
misaada tena yenye mashariti, Kwanini wahisani hao wasitowe misaada bilaya
mashariti kama kweli wanaipenda Malawi, Je serikali ya Malawi inasindwa kujua
hili?. Kitu kigine ni pale serikali ya Rais Joyce Banda kukwepa kua mwenyeji wa
mkutano wa Afrika iki hofu kwamba Rais Ommar Al-Bashir wa Sudani angeuzuria hivyo basi serikali yake
ingekosa misaada kutoka nchi wahisani, ukizingatia hayo kuna uwezekana Rais
Joyce Banba akatumiwa na nchi za kigeni ili alete chokochoko katika Ziwa Nyasa
akilubuniwa kwa misaada . kuna mambo mengi yana semwa, wengine wana amini
kwamba Malawi anapewa jeuri na Muingereza kwani hata kampuni iliyo pewa leseni
ya kutafiti gesi na mafuta ni ya Uingereza ijulikanayo kama SURESTREAM hivyo basi tusi pandishe
jaziba bila ya kujua nyuma ya pazia kunanini. Lengo si kuogopa eti Malawi
anasaidiwa nanani bali ni kutaka kutafuta njia madhubuti ya kumshinda kwa
lolote litakalo tokea.
Serikali ikumbuke yaliyo tokea miaka ya
sitini (1960s), katika kipindi hiko Rais wa Malawi Hastings Kamuzu Banda na
Mwalimu Nyerere wa Tanzania walishindwa kupata suluhu ya tatizo kuhusu hata
jina tu la Ziwa hilo, je tuna hoja gani mpya ukiacha zile za mwalimu Nyerere
ambazo zilishindwa kuzaa matunda. Ilifika wakati Rais Hastings Kamuzu Banda
alisikika akidai kuwa maeneo ya Songea, Kyela na Njombe yalikua sehemu ya nchi
ya Malawi,alikua akidai ya kwamba alipatiwa kumbukumbu(Ramani) na Baba yake,
hali hiyo ilitaka kusababisha vita kali kati ya Tanzania na Malawi mwaka 1968.
Mkataba ambao Malawi wanautumia kama nyenzo
ulikua na lengo la kuonyesha kwamba nchi hiyo ilikua nchini ya Uingereza na
Tanzania chini ya Ujerumani, Nimekua nikishangazwa na Serikali ya Malawi
kukosa umakini katika mzozo wa Ziwa
Nyasa, mfano ni pale wanapo jichanganya katika kutumia Azimio la Umoja wa
Afrika la mwaka 1963,linalo taka nchi wanachama wa Africa kukubaliana na mipaka
iliyopo, hili si jambo baya lakini wakumbuke kwamba katika ibara ya sita ya
Heligoland Treaty wa 1890 ambao ni msingi wa madai yao unabainisha
kwamba nchi zinazo husika zikutane na kurekebisha kasaro katika mazingira
yatakayo lazimu, je wamalawi hawalijui hili au kwa nini hawalisemi hili?,
waache kutumia Azimio la Afrika la mwaka 1963, na 2002,2007 ilihali wakiwa hawa
zingatii ibara ya sita ya mkataba( section six of Heligoland Treaty/
Anglo-German Agreement) wa mwaka 1890. Ninge penda serikali iwaulize Malawi
hivi kweli mkataba huo ulikua halali kwa Tanzania?( Was it legitimate?) kwa
sababu Tanzania( Tanganyika before the Indepence) haikushiliki katika kuandikwa
kwa mkataba huo wa mwaka 1890.
Mzozo kama huu si wa kwanza kutokea dunian,
Tanzania haipaswi kuyumba katika mzozo huu kwani isha wai kutokea sehemu
mbalimbali za dunia, mfano safi ni hapahapa barani Afrika baina ya CAMEROON na NIGERIA kuhusu mpaka wao katika ziwa chad katikati ya Nigeria na
Cameroon, baada ya kushindwa kupata suluhisho wali kwenda kwenye mahakama kuu
ya Dunia, na hivyo basi ika amuliwa mpaka upite katikati ya Ziwa Chad ukifuata
msitari ulio nyooka (A median Line). Dunia inatambua kwa nchi mbili zinazo
tenganishwa na maji mpaka wake ni katikati (
Where there is shared water body the border is at the middle) ikimaanisha zina tenganishwa na msitari ulio nyooka
ujulikanao kama MEDIAN LINE. Kwa kuzingatia mfano huo na mingine duniani
serikali yetu lazima ijipange madhubuti kuishinda Malawi, Historia inaonyesha
kwamba hakuna ‘’case’’ ( mgogoro) kama huu duniani ambao umme amuliwa kwa kwa
nchi moja kupewa Ziwa au Mto wote kitaalamu ijulikana kama ( One hundred
percent monopoly) bali, suluhisho utolewa kwa kwa kuangalia asilimia hamsini,
kitaalamu ujulikana kama (Fifty percent solution)
Kama tutakwenda mahakama ya dunia tuzingatie
vigezo muhimu, kuna vitu muhimu ambavyo mahakama ya dunia inazingatia
katika mizozo kama huu wa Ziwa Nyasa, kwanza serikali husika lazima iwe na
takwimu sahihi( correct details) kutoka kwa wakazi wa eneo husika na vyanzo
vingine, hivyo basi lazima serikali ipate taarifa kutoka kwa watu
wanaolizinguka Ziwa Nyasa kwa Upande wa Tanzania ili waweze kutoa uthibitisho
utakao saidia kupambana na Malawi.Kingine ni kwamba Serikali lazima itambue na
isimamie ya kwamba Mkataba wa mwaka 1890( Heligoland Treaty/ Anglo-Germany
Treaty) ulikiuka sheria na mila za
kimataifa,kitaalamu inajulikana kama( Customary International law) kwa sababu
hauku zingatia haki za wakazi wa eneo hilo, kama vile tamaduni zao na maisha ya
kila siku. Haya yote yanatosha kuipiku Malawi katika kulipigania Ziwa Nyasa.
Tusisahau kuwakumbusha Malawi mambo haya,
Serikali yetu lazima itowe taarifa kwamba mwaka 1928 wakati wa utawala wa
Donald Cameroon ambae alikua Gavana wa pili wa Tanganyika, alikutana na Gavana
wa Nyasaland ili kubadilisha mpaka wa nchi hizi mbili na kuwawezesha wakazi wa
pande mbili kutumia Ziwa Nyasa bila tatizo, swala hilo halikuzingatia mkaba wa
mwaka 1890 ambao ulikua na lengo la kuizuia Ujerumani kutotumia Ziwa Nyasa na
sio kuwapo kwa mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland, hivyo basi kwa kuwa
mjeruman alinyang’anywa Tanganyika na kuwa
kwenye himaya ya muingereza kama ilivyokuwa kwa Nyasaland(Malawi)
magavana hao walikubaliana mpaka upite katikati ya Ziwa Nyasa kwakua nchi zote
mbili zilikua kwenye utawala wa muingereza.
Tusiwe watumwa wa nchi za kigeni kutoka
Asia au Amerika, Tanzani lazima itambue umuhimu wa mipaka yetu, isitokee
nchi yoyote iwaka inataka tutuingilia katika maamuzi ya nchi yetu, tusikilize
ushauri wao lakini wasiwe na lengo na kutaka kufanikisha masilahi yao, dunia
sasa ipo katika vita ya kutafuta mafuta na nishati nyingine kama gasi ( Oil
imperialism) inayo ratibiwa na Nchi kubwa duniani kama vile Uingereza na Marekani
pamoja na Zile Zinazokuwa kwa kasi kiuchumi. Kama wakijuwa Ziwa Nyasa kuna
hivyo vitu(Mafuta na Gesi), wanaweza kuvaa ngozi ya kondoo wakati wao ni chui
kwa lengo la kufanikisha mahitaji yao, Swala hapa ni mpaka kati yetu na Malawi,
kwani Tanzania inahaki kama nchi nyingine kulinda mipaka yake bila ya kujali
kama kuna mafuta na gesi au la,lazima tuijulishe Malawi na dunia yote kwamba, tunapigania Ziwa Nyasa si kwa sababu
ya mafuta au gesi bali ni mpaka wetu ambao ni muhimu kwa maendeleo na amani ya
nchi yetu.Mwandishi mjoja wa maswala ya mipaka JEAN
BLANCHARD aliwai kusema hivi, ‘Boundaries are external assets to
surmount domestic deficiencies’’ hivyo basi kulinda na kupigania mipaka yetu
haisababishwi na kuwapo kwa mafuta au gesi.Malawi lazima itambue kwamba atakama
ikitokea sehemu nyingine tutapigania mpaka wetu bila ya kujali kuna nini,kama
swala la gesi Malawi itambue kuwa, Mnazi bay, songosongo na maeneo ya Zanzibar
kumegundulika gesi nyingi sana ambayo wao hawana hata theluthi yake, swala letu
na wao ni mpaka. Watanzania wapatao laki sita 600,000
waliopo eneo hilo wanapaswa kulitumia Ziwa Nyasa kwa kuamini kwamba Ziwa hilo
ni Triple heritage, ambapo wakazi wa Msumbiji, Malawi na Tanzania limekuwa
zawadi kwao kwani limewazunguka kila mmoja, hali inayosababisa mpaka wake uwe
katikati ya ziwa hilo.
Imeandaliwa na Suleman A Kuchengo
Mwanafunzi mwaka wa tatu,
Digrii ya Uhusiano
wakimataifa(International Relations).
Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
0714937641/suleykuchengo@yahoo.com
Post a Comment