| Karandika lililobeba mahabusu wengine likiwasili mahakamani hapo bila ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi |
| Askari polisi wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha leo |
Mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi , |
Wanahabari wakiwa wamejipanga kwa picha wakisubiri mtuhumiwa kuletwa mahakamani hapo
SAKATA ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limeendelea kuchukua sura mpya mkoani Iringa baada ya askari polisi anayetuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo kufichwa katika gari maalum na askari wenzao .
Tukio hilo lilitokea leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani huku askari
polisi hao muda wote walionekana kuzunguka huku na kule katika
mahakama hiyo kama njia ya kuwathibiti wanahabari waliokuwepo
mahakamani hapo wasipate nafasi ya kumpiga picha mtuhumiwa huyo
.
Zikiwa
zimebaki kama dakika 10 mahakama kuanza
gari hilo lilisogea hadi mlango wa Mahakama na askari waliokuwepo
mahakamani hapo zaidi ya 20 kulizunguka gari hilo huku wengine
wakiwathibiti wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi kama njia
ya kuzuia kupigwa picha kwa mtuhumiwa huyo na baada ya kuingia ndani ya
mahakama kabla ya hakimu kufika uthibiti ndani ya chumba cha mahakama
ulikuwa mkali zaidi dhidi ya wanahabari hasa wale wenye kamera.
Wakati huo huo Mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa imeahirisha kesi hiyo ya mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi ambae pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) ,mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573 Simoni (23) atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5 mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena.
Post a Comment