Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe
iwasili stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha
Majumbani Kwao. Baadhi ya Abiria wakiwa wamewahi kwaajili ya Kupanga
foleni ili waweze kupata siti huku wengine wakichuchumaa kutokana na
kulisubiri kwa muda
Abiria Wakiteremka katika treni linalofanya safari zake ndani ya Jiji la
Dar mara lilipowasili Katika Kituo cha Stesheni karibu na central
polisi tayari kwa safari ya kurudi tena Ubungo
Baadhi ya Abiria waliogeuza na treni hilo wakiwa wamepandia Kituo cha
Kamata Ili kuwahi Siti ambapo walipelekea sintofahamu kwa baadhi ya
abiria waliokuwa kituoni hapo na kutaka kupanda kwenye hilo behewa
kukuta likiwa tayari limeshajaa kutoka na abiria kugeuza na treni hilo
wakati utaratibu huwa haurusiwi na ikifika mwisho abiria wote wanatakiwa
kushuka
Abiria wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya
treni la mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na
moja na dakika ishirini jana
Mmoja wa Abiria aliyegeuza na treni hilo ambapo walipandia Kamata kwa
lengo la kuwahi kiti akibishana na mmoja katika ya abiria ambao walikua
kwenye foleni muda mrefu wakisubiria treni hilo kufika ili waweze
kuingia ndani na kupata siti ambapo alikuta behewa hilo likiwa
limeshajaa na kuanza kubishana huku abiria waliokuwa wakisubiri treni
hilo wakitaka abiria waliogeuza na treni hilo kushuka
Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa
jina la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika
kituo cha Stesheni tayari kwa kurudi nalo ubungo huku baadhi ya behewa
kuwa limeshajaa kabla hata halijafika kituoni hapo kutokana na abiria
kugeuza nalo kwa lengo la kuwahi siti. Behewa ambalo lilikuja likiwa
limeshajaa ni behewa lenye namba 3644 ambalo abiria wake walikua
wamepandia njiani kwa nia ya kugeuza nalo ili waweze kupata siti.
Wakazi wa jiji la Dar wakipanda kwenye treni la mwakyembe mara baada ya
kuwasili kwenye kituo chake cha Stesheni jana Kwenye majira ya Saa 11
Jioni jana tayari kwa kuwarudisha majumbani kwao likitokea Mjini
kuelekea Ubungo ambapo ndio kituo cha Mwisho
Na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
Katika hali isiyo ya kawaida jana kwenye majira ya Saa 11: 20 Jioni
katika kituo cha Treni kilichopo stesheni mkabala na Kituo Cha Polisi
Cha Cetral kuliibuka Jambo la kushangaza wakati abiria wanaosubiria
treni inayofanya kazi zake ndani ya jiji la dar kuona behewa moja likiwa
limeshajaha tayari kutokana na abiria kupandia njiani na kugeuza nalo
kwa lengo la kuwahi siti na kupelekea abiria waliowahi kituoni hapo na
kupanga foleni kwaajili ya kuwahi siti kuambulia patupu.
Abiria waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika pale ambapo
walikuta behewa hilo limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika kwenye
kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi .
Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya
wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo
ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo
waneshaanza kuchakua kitu ambacho utaratibu hauruhusu.
Utaratibu uliopo ni kwamba hata kama abiria amepandia katikati anatakiwa
kuteremka pindi treni hilo linapofika mwisho wa kituo ndipo akate
tiketi kwaajili ya kupanda tena na kurudi nalo lakini hali imekuwa
tofauti hapo jana baada ya abiria hao kutokushuka na tiketi kukatiwa
ndani na kupelekea abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo kusubiri kwa
muda mrefu.
Lukaza blog imeweza kunakili sauti za abiria ambao waliokuwa
wakilalamika juu ya utaratibu huo uliofanywa na wafanyakazi ambao sio
waaminifu na kupelekea usumbufu kwa abiria ambao wamewahi kupanga
foleni.
Post a Comment