Mgogoro Wa Ardhi Kapunga - 6






Walivyoshiriki kuutafuna Mradi wa Mpunga Kapunga


"TUNAWEZA kujibagua kutoka kwa wenzetu kutokana na elimu tuliyonayo; tunaweza kujaribu kujilimbikizia wenyewe mali haramu ya umma. Lakini gharama kwetu, pamoja na kwa ndugu zetu, itakuwa kubwa mno. Itakuwa kubwa siyo tu kwa kushindwa kutimiza haja zetu, lakini pia kwa usalama wetu na ustawi wetu." Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Nyerere yaliyomo katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo cha mwaka 1973.
Nimeona bora nianze na maneno haya ya Mwalimu Nyerere katika kuelezea kilichotokea katika Mradi wa Umwagiliaji wa Mpunga Kapunga, ambao kwa hakika kama ungeendelezwa vyema, ungekuwa mkombozi mkubwa kwa taifa katika suala zima la chakula.
Muundo wa uongozi katika mradi huo ulikumbwa na mabadiliko kadhaa wakati wa uanzishwaji wake, ambapo kulionekana kuwa na “taasisi” mbili – Idara ya Operesheni na Ukarabati na Kamati ya Menejimenti, nyongeza ambayo hata wafadhili wenyewe wa mradi huo hawakuwahi kuiwaza kabla ya kuidhinisha mkopo.
Idara ya Operesheni na Matengenezo iliongezwa Julai 1990 kwa lengo la kushughulikia ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji, majengo na kazi nyingine za ujenzi. Kuwepo kwake kulisaidia ukarabati wote katika kipindi hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post