
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe yupo kwenye kitimoto baada ya serikali
 yake kuwa na mipango ya kuhamisha mji mkuu kutoka Harare hadi kwenye 
wilaya anayotokea, mpango ambao viongozi wa upinzani wanasema 
hawakushirikishwa.
Waziri wa serikali za mitaa Ignatius Chombo wiki hii alidai kuwa 
mipango inaendelea kujenga jengo jipya la bunge, ofisi za serikali, 
ikulu na nyumba za kukaa huko Mt Hampden, takriban kilomita 40 magharibi
 mwa Harare ili uwe mji mkuu mpya.
Bwana Chombo alisema uamuzi huo ni kupunguza mlundikano wa watu jijini Harare ambako kuna zaidi ya watu milioni 1.6.
Jiji lililopendekezwa ni katika wilaya ya  Zvimba ambayo ni wilaya ya
 Mugabe na pia hupata fedha zaidi za maendeleo kutoka serikali licha ya 
kuwa na wakazi wachache.
Makampuni ya kichina ambayo huhusika na uchimbaji almasi na ambayo 
yamewekeza kwenye mahoteli na shopping malls nchini humo yanatarajiwa 
kupewa ukandarasi wa mradi huo mpya.
Wananchi wengi wa Zimbabwe wanahoji mantiki ya kujenga jiji jipya 
wakati maeneo mengi ya mjini yanadorora kutokana na matatizo ya kiuchumi
 yaliyodumu kwa kipindi kirefu.
Wilaya ya Zvimba  tayari inaongoza kwa kuwa na barabara bora nchini humo na makazi mengi yana umeme.
Post a Comment