| Mashabiki wa Yanga wakiandamana na vigoma na vuvuzela katikam maeneo ya stendi kuu ya mabasi jijini Tanga leo ikiwa ni mikwara yao kabla ya kuwavaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jioni. |
Mechi kali ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara
itakayokuwa ya kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo kati ya wenyeji
Coastal Union na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo
jioni imeandika rekodi baad ya tiketi zake kuuzwa kwa bei 'mbaya' kuliko
mechi zote za msimu huu ikiwamo ya mabingwa watetezi, Simba dhidi ya
wenyeji hao (Coastal).
Mauzo ya tiketi hizo leo ni Sh. 5,000 kwa kiingilio cha chini (ambazo kufikia saa 9:00 watu walikuwa wakizilangua kwa Sh. 7,000), Sh. 10,000 na Sh. 15,000 kwa kiingilio cha juu wakati katika mechi nyingine zenye mvuto zaidi ikiwamo ya Simba dhidi ya Coastal, viingilio vilikuwa Sh. 4,000, Sh. 7,000 na Sh. 10,000.
Licha ya viingilio hivyo vikubwa, mashabiki walionekana wakichangamkia tiketi hizo kwa wingi, wengine wakitokea jijini Dar es Salaam na baadhi katika maeneo ya jirani ya jiji la Tanga kama Kabuku, Mwakidila, Duga Maforoni, Pangani, Muheza, Korogwe na kwingineko.

Post a Comment