
Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake
“Are you ready for Mexico? Are you ready for tequiiiiiiila? Sit down,
buckle your seat belts, and let’s get drunk,” ni sauti ya Rihanna
inayosikika kwenye ndege ya Boeing inayomzungusha kwenye ziara yake
aliyoipa jina la 777. 777 maana yake ni siku 7 za tour katika majini 7
ya nchi 7 duniani.
Wakati ndege ikiwa angani mashabiki wa Rihanna waliopata bahati ya
kualikwa kwenye tour hiyo pamoja na waandishi wa habari wapatao 150
kinachooendelea ni kula bata na mtungi kwa kwenda mbele.
Katika wakati mmoja safari hiyo iliingia dosari kidogo baada ya
mwandishi mmoja kuamua kuvua nguo zake wakati ndege ikiwa hewani na
kuamsha kelele na shangwe nyingi kwenye ndege hiyo.
Safari hiyo imeingiwa na dosari baada ya Rihanna kukataa kufanya
interview na mwandishi yeyote na kumfanya mtangazaji huyo wa Fox FM ya
mjini Melbourne, Australia kuvua nguo zake.
Wengine wanalalamika kuwa Rihanna amekuwa akitumia muda mwingi
amejifungia kwenye chumba cha dharura.Pia huduma ya chakuka kwenye ndege
hiyo imekuwa ikilalamikiwa na watu hao wanaodai kulishwa vyakula vya
ajabu ajabu.
Wengine wanadai kuwa hawana muda wa kupumzika licha kufikia kwenye
hoteli za kifahari ambako hulala kwa saa mbili au tatu tu kabla ya
kuamshwa tena kuanza safari ya nchi nyingine.
Leo Rihanna atakuwa na show jijini London na tayari ameshaperfom Mexico City, Toronto, Stockhom, Berlin na Paris.
Hizi ni baadhi ya picha za ndani ya ndege hiyo na zile anazotumbuiza kwenye ziara hiyo.
- Rihanna akiwa na marubani wa ndege ya tour yake
- Rihanna akiwa na furaha ndani ya ndege kama vile ametoka kuongea na Chris Brown kwenye simu
- The beautiful Rihanna
- Rihanna kwenye stage
- Akiwa uwanja wa ndege baada ya kuwasili
- Rihanna, mashabiki wake na waandishi wa habari wakifurahia safari
- Take as many photos as you can!!
- Rihanna akiperform mjini Stockhom Sweden



















Post a Comment