SERENGETI BOYS YAUA, YAMPIGA MOJA BILA CONGO(ANGALI MWANZO MWISHO KATIKA PICHA TAIFA LEO)


Kipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ya Kongo Brazzaville, Ombandza Mpea Joe akilalama baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Mufathir Yahya Abbas kutinga nyavuni na kuwapa wenyeji ushindi wa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Bao pekee leo

Kipa wa Kongo akining'inia kwenye milingoti ya lango baada ya kuukosa mpira uliopaa juu ya lango lake

Mchezaji wa Serengeti, Suleiman Hamisi Bofu akipiga mpira kichwa mbele ya beki wa Kongo, Ondongo Boungena

Beki Okombi Francis wa Kongo akiokoa mbele ya Joseph Kimwaga 

Wachezaji wa Kongo wakimdhibiti mchezaji wa Serengeti

Hussein Twaha 'Messi' akiwafunga tela wachezaji wa Kongo

Makocha wa Serengeti Jacob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo wakiwapa maelekezo vijana wao wakati mpira uliposimama kwa muda

Kipa wa Serengeti Boys, Peter Manyika akiruka hewani kupangua mchomo mkali ulioelekezwa langoni mwake 

Kipa wa Kongo, akimdondokea kiungo wa Serengeti, Farid Mussa Shah kudaka mpira, huku beki wake, Ondongo Boungena akiwa tayari kumsaidia 

Farid kulia na Ondongo kushoto

Kikosi cha vijeba wa Kongo Brazzaville

Beki Ismail Adam Gambo wa Serengeti akimdhibiti Ibara Vinny wa Kongo Brazzazille

Hussein Twaha akiwatoka wachezaji wa Kongo

Serengeti wakishangilia bao lao kwa staili ya aina yake

11 wa kwanza wa Serengeti leo

Wachezaji wa Serengeti Boys wakiimba wimbo wa taifa

Benchi la Ufundi la Serengeti Boys wakati wa wimbo wa taifa

Hussein Twaha akipasua katikati ya msitu wa wachezaji wa Kongo

Hussein Twaha akimiliki mpira mbele ya beki wa Kongo

Joseph Kimwaga akimtoka beki wa Kongo Brazzaville


Beki wa Kongo Okombi Francis baada ya kumpitia kwanja Tumaini Baraka Mosha wa Serengeti
Mudathir akiondoka na mpira

Tumaini Baraka Mosha akimtoka Okombi

Kushoto refa anasema twende, huku Tumaini Baraka Mosha akiwania mpira dhidi ya Ondongo
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeifunga  1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu na ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za vijana wa umri huo Afrika zitakazopigwa nchini Morocco mwakani.
Kwa matokeo hayo, Serengeti sasa inahitaji hata sare yoyote katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo mjini Brazzaville ili kukata tiketi ya Morocco mwakani.
Kwa ujumla Serengeti walipigana katika mchezo wa leo, kwani wapinzani wao walionekana kuwa bora na wenye uzoefu zaidi yao.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Miiro Nsubuga, aliyesaidiwa na Mark Ssongo, Balikowa Ngobi na Ronnie Kalemba wote kutoka Uganda, hadi mapumziko Serengeti walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililopatikana dakika ya 15.
Bao hilo lilifungwa kwa shuti la mpira wa adhabu na beki Mudathir Yahya Abbas kutoka umbali wa mita 22 na mpira kabla ya kutinga nyavuni ulimbabatiza beki mmoja wa Kongo na kumpoteza njia kipa Ombandza Mpea Joe na kujaa nyavuni.
Faulo hiyo ilitokana na kiungo wa Serengeti, Hussein Twaha Ibrahim ‘Messi’kuangushwa na beki Okombi Francis wakati akiwa analekea kwenye eneo la hatari la Wakongo.
Baada ya bao hilo, Wakongo walijaribu kuongeza jitihada kiuchezaji, lakini ukuta imara wa Serengeti ulioongozwa na kipa Peter Manyika uliwazuia kusawazisha hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatimia.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Serengeti Boys, Mdenmark, Jacob Michelsen aliwapongeza vijana wake, lakini akasema bado wana kazi kubwa mbele yao.
Kocha wa Kongo, Mfaransa Eddie Hudanski alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88, baada ya awali kuonywa kwa kutoa lugha chafu, lakini akarudia.
Refa Nsubuga alitoa kadi moja tu ya njano kwa Issambey Lonvreve aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ibara Vinny.
Tanzania; Peter Manyika Peter, Miza Kriston Abdallah, Mohamed Hussein Mohamed, Ismail Adam Gambo, Miraj Adam Suleiman, Mudathir Yahya Abbas, Mohamed Salum Haroub, Joseph Kimwaga Lubasha/Dickson Isaac Ambundo, Hussein Twaha Ibrahim, Suleiman Hamisi Bofu/Tumaini Baraka Mosha na Farid Mussa Shah.
Kongo Brazzaville; Ombandza Mpea Joe, Tmouele Ngampio, Mabiala Gharlevy, Okimbi Francis, Ondongo Boungena, Ibra Vinny/Issambey Lonvreve, Binguila Handy, Obassi Ngatsongo, Mohendiki Brel, Atoni Mavoungou na Biassadila Arei. 
Picha na Bin Zubeiry

Post a Comment

Previous Post Next Post