
Kwa muda mrefu aliyekuwa member wa kundi la East Coast Team, ECT, rapper Snare, amekuwa kimya na shughuli za muziki lakini ameamua kuelekeza nguvu zake kwenye filamu.Kwa sasa Snare ni mtayarishaji wa filamu chini ya kampuni iitwayo Afronode Film na December 1, 2012 anatarajia kuzindua filamu iitwayo SHUJAA…check out trailer yake hapa
Hii ni story fupi ya movie hiyo:
Amani ni mmoja wa vijana aliyeguswa na kitendo cha Raisi JAKAYA
MRISHO KIKWETE cha kuamua kupima VVU hadharani. Naye kuanzia hapo
alijiwekea utaratibu wa kufanya hivyo kila baada ya miezi mitatu, na kwa
bahati nzuri alikuja kufanya kazi katika shirika linaloshugulika na na
kupima VVU na Ushauri nasaha.
Siku moja alikutana na binti mzuri Fransisca akiwa katika mazingira
ya kujiuza (changudoa). Alimuona ni mzuri sana akampenda, na akataka
kujua zaidi. Hadithi ya maisha ya yule msichana ndio yanamfanya amani
awe na imani zaidi. Lakini jambo moja linatatiza kati yao je yule
msichana ni salama? hakuna kinachoweza kufumbua fumbo hili zaidi ya
kwenda kupima kitu ambacho Francisca hakuwa tayari kutokana na idadi ya
wanaume aliotembea nao.
Ugumu wa jambo hilo haumkatishi tamaa amani, hatimaye anafanikiwa
kuokoa maisha ya msichana huyo. Na kutimiza ndoto zake za kuwa shujaa
kama Raisi Jakaya Kikwete.
Post a Comment