Spika wa Bunge Anne Makinda akisoma taarifa Bungeni mjini Dodoma leo juu ya ripoti ya tuhumu za rushwa zilizowakabili wabunge kadhaa.
Na.Mwandishi wetu, Dodoma.
Wabunge waliotuhumiwa  kwa kujihusisha na rushwa leo wamesafishwa na Spika Anne Makinda baada ya kutoa ripoti aliyosoma  leo  iliyoshindwakudhibitisha  kuwa wabunge hao walikuwa wamekula rushwa.
Kutokana na ripoti hiyo imemlazimu Spika kukemea tabia ya baadhi ya wabunge kuwatuhumu watu au wabunge wengine juu ya  rushwa wakati wakichangia hoja bungeni.
Akitoa uamuzi wake Spika Anna Makinda alimewapa onyo wabunge waliotoa matamko ya rushwa wakiwa wakichangia  hoja bungeni.
Spika pia amewapa onyo kali Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu  Maswi na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Soppter Muhongo kwa kuwazushia tuhuma za rushwa wabunge kadhaa.
Spika Anna makinda amelaumu tabia hiyo ya kuwatuhumu wabunge kuhusiana na Rushwa.
Baadhi ya wabunge hao walitajwa na ripoti ya Spika Anna Makinda kwamba wamejihusisha  na rushwa ni pamoja na wabunge wa Viti Maalum, Saraha Msafiri  Ali na Munde Tambwe.
Wengine ni Mbunge  wa Bukene (CCM),  Selemani  Zedi , Mbunge wa Simanjiro (CCM) , Christopher Ole-Sendeka na  Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA).
Mbunge Sarah Msafiri (wa kwanza kushoto) aliyetuhumiiwa kuomba rushwa ya Sh Milioni 50 kutoka kwa Katibu  Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, akiwa bungeni na wenzake wakati ripoti ya Spika akisoma leo bungeni.