![]() |
Wapenzi wa muziki wa Hip hop wakifutailia burudani jana |
Tamasha maalum kwa ajili ya wana Hip Hop na Rap kwa kutumia
ghani na lafudhi ya Kiswahili also known as “Swahili Hip Hop Summit”
jana ilizinduliwa rasmi katika kituo cha utamaduni cha watu wa Ufaransa,
Alliance Francaise na kukonga nyonyo za watu waliojitokeza.
Tamasha hilo ambalo limeandaliwa maalum kama sehemu ya maonyesho ya
kazi za wasanii wa Hip hop ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika
kubaguliwa na kutengwa lilipata ugeni wa waheshimiwa mabalozi wa
Ufaransa na Uswisi majira ya saa 4 asubuhi, ambapo walitembelea na
kukagua kazi mbali mbali za kisanii zinazoonyeshwa katika ukumbi wa
mikutano na matukio katika kituo hicho cha utamaduni.
Tamasha hilo limegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni
maonyesho (exhibition) na burudani(entertainment), huku likifuata
misingi mikuu ya nguzo tano za Hip hop ambazo ni pamoja na kughani
mitindo huru (Free Style), Kucheza Dance kwa Mitindo huru (Break
Dance), Sanaa ya uchoraji kwa kutumia makopo ya rangi ( Grafitti),
Kuonyesha uwezo wa ku Dj ( Dj-ing), na ujuzi ama uelewa wa elimu ama
misingi ya Hip-Hop.
Kwa asilimia kubwa maonyesho hayo yanaonekana kukubalika zaidi na
wasanii wa hip hop toka Arusha ambao kwa jana walikuwepo wengi zaidi.
Bidhaa mbali mbali toka makundi tofauti ya wasanii toka Arusha wakiongozwa na JCB zilikuwepo katika maonyesho.
Aidha katika tamasha hilo, vipengele vya mitindo huru (free Style)
ilitawaliwa na vijana wawili ambao ni leloo na Mtaganda, wakati Dj-ing,
na Break dance ikitawaliwa na wakongwe wawili wa zamani katika fani
hizo Bwana Diga Diga ambaye anajulikana zaidi Double D na katika fani ya
Break Dance na John Dilinga ambao waling’ara na kuamsha shangwe za mara
kwa mara kwa uwezo mkubwa walionyesha katika fani zao.
Tamasha hilo linaingia siku ya pili leo, ambapo kutakuwa na maonyesho
na burudani zaidi mida ya jioni huku ikitarajiwa kuhutubiwa na balozi
wa Ufaransa nchini Bwana Marcel Escure.
Credit:- bongo5.com
- Msanii wa kughani mitindo huru Leloo akifanya vitu vyake
- Mtaganda akimchana Leloo, palikuwa hapatoshi
- Mtaganda kizidi kupigilia misumari ya free style kwa leloo
- hapa Mtaganda alijisahau akapiga hadi kiingereza
- De Fashion Girls wakiwa na Mangi Mweusi Heriel, ambaye ni mtaalamu wa graffiti
- Fish Masamaki akionyesha zana yake ya kazi baada ya kumaliza kuchora
- Heriel akionyesha utundu wake wa kuchora kwa style ya Grafiti
- Heriel akiuza sura baada ya kazi
- Wataalamu wawili wa Grafitti Fish Masamaki na Heriel waki shoo love pamoja
- Jcb na Kekuu wakishoo love
- JCB akishoo love na fan wake
- Nguzo mbili za hip hop Rap na Grafiti…No introduction hapo
- Ilikuwa ni mikuno ya kwenda mbele toka kwa Dj JD
- Jd Alifunikaaa bovu
- Da Legend Is Back with full ma tekniki.
- Hapo ilikuwa ni ku dj na kumix na kuweka machines sawa.
- Utu uzima dawa jamani Break dancer wa zamani Double D akizunguka
- Hapa sitii neno, subiri video yake ujionee mwenyewe
- Unene haukumsumbua kabisa kujiachia stejini
- Diga diga alitisha ki ukweli maaana alipopiga hii watu ndio wakamvulia kofia kabisa.
- Vitu vya kina Buga Lou na Shebby Do
- Diga Diga ni mfano wa kuigwa.
Post a Comment