Meneja
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la
Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi
vya DStv likaloanza hapo kesho, ambapo amesema punguzo hilo
litawawezesha wateja wao kulipia huduma za Matangazo ya Televisheni ya
kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema Offer hiyo ya Punguzo la bei
ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kuelekea
katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulia
ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Barbara Kambogi na Kushoto
ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu.
Meneja
Masoko wa Multichoice wa Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa
ufafanuzi kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea matumizi ya mfumo wa
Digitali DStv kwa kuwajali wateja wake imepunguza gharama za
kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za Kitanzania 169,000 unaweza
kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Barbara
Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa DStv kuwa sasa
kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya hali ya juu na
kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya kuunganishwa ili
watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya kuelimisha na
kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo mbalimbali
katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu ndio sasa muda
muafaka kwa kujipatia DStv.
Meneja
Mauzo wa DStv Tanzania Bw. Salum Salum akifafanua kuwa Multichoice
imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wateja ambapo sasa wanamawakala 200
nchini na kuwataka wanapokwenda kulipia Ving’amuzi vyao ni lazima
wahakikishe vimewashwa ili kurahisisha kufanyika kwa huduma hiyo pia
amesema wateja wa DStv wanaweza kufanya malipo ya huduma hiyo kupitia
simu za mkononi na ukizingatia kampuni hiyo imeongeza maeneo ya kutoa
huduma ikiwemo Uchumi Super Market, Kariakoo na Mlimani City kwa wakazi
wa Dar es Salaam.
Kampuni
ya MultiChoice imetangaza punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa
wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv litakaloanza kesho Novemba
15, 2012.
Meneja
Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo
litawawezesha wateja wao kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya
kituo hicho kwa gaharama nafuu.
Fauel
alisema kwa wateja watakaokuwa wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya
mwezi huu, wataendelea kutumia hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha,
kisha wataanza na bei mpya ya punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila
wahakikishe huduma yao kutokatika.
“Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida,” alisema Fauel.
Meneja
mkuu huyo alisema, kuwa kama kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa
bei kulingana na kipato chao, hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa
kiwango kikubwa ili kila mmoja afaidi burudani.
Alisisitiza
kuwa DStv itaendelea kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla
vipindi vyenye ubora kwa vile wamewekeza katika vipindi vipya.
Kwa wateja watakaonufaika na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000 kwa mwaka!
Fauel
akaongeza kwamba “Tunawaahidi wateja wetu huduma bora na kwamba kwetu
mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa usambazaji unazidi kupanuka na sasa
tupo kila mkoa wa nchi. Pia tunafurahi kwamba sasa tuna ofisi zetu
Kariakoo na supermarket ya Uchumi iliyopo barabara ya Pugu. Hii
itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa na huduma zetu kwa haraka
zaidi.
Habari na MoBlog




Post a Comment