Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa
Na Mwandishi wetu
Hivi karibuni Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EUC) na
Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi wa Umoja huo walikutana jijini
Brussels, Ubelgiji kujadili Bajeti ya mwaka 2013 ya umoja huo, ambapo
walitangaza masharti mapya ya utoaji misaada kwa nchi zinazoendelea.
JUMUIYA ya Ulaya (EU), imeongeza masharti kwa
Serikali ya Tanzania ili iweze kupatiwa msaada wa Bajeti kwa mwaka ujao
wa fedha 2013/14.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili
imezipata, masharti mapya yaliyotolewa na jumuiya hiyo ni pamoja na
kuitaka Serikali ya Tanzania kusimamia kikamilifu masuala ya haki za
binadamu, utawala wa sheria, kuwapo mfumo madhubuti wa uwajibikaji
katika usimamizi wa Bajeti na ushirikishwaji wa taasisi huru.
Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini,
Filiberto Ceriani Sebregondi alibainisha hayo jana katika mawasiliano na
gazeti hili kwa njia ya mtandao kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba
Wahisani Wakuu wa Bajeti ya Serikali (GBS), wamechelewa kuwasilisha
fedha hizo katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha nchini.
Balozi Sebregondi alitaja maeneo mengine yaliyosisitizwa na EU kuwa ni pamoja usimamizi sahihi wa rasilimali za taifa na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa Serikali.
Balozi Sebregondi alitaja maeneo mengine yaliyosisitizwa na EU kuwa ni pamoja usimamizi sahihi wa rasilimali za taifa na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa Serikali.
Alisema kuwa kikao cha mwaka cha mapitio ya
uchangiaji wa Bajeti ya Serikali kilichofanyika wiki iliyopita
kilichowahusisha wachangiaji wakubwa wa GBS, ikiwamo EU na Serikali ya
Tanzania kiliweka wazi juu ya kuwapo kwa uboreshaji wa mfumo wa utoaji
msaada na kuridhiwa na pande zote.
Balozi huyo alisema, “EU kupitia chombo cha kutoa
msaada wa kibajeti, mara kadhaa imekuwa ikifanya majadiliano na
Serikali ya Tanzania juu ya kuongeza juhudi katika kuleta mabadiliko
yakinifu kwenye maeneo ya uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa.
“Wiki iliyopita wachangiaji wa GBS ikiwamo EU,
walikutana na Serikali ya Tanzania kufanya tathmini ya mwaka wa fedha
uliopita na kufikia makubaliano juu ya mabadiliko ya mfumo wa utoaji
misaada kwa nchi zote zinazofadhiliwa.
Alipoulizwa kuhusiana na masharti hayo jana,
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alikiri kufanyika kwa mazungumzo
baina ya Serikali na wahisani na kwamba waliyapokea na wapo tayari
kuyatekeleza.
Waziri Mgimwa alisema, “Masharti hayo hayana athari yoyote kwa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha ujao wa 2013/14.”
Alisema kuwa hadi sasa Serikali inaendelea vyema
na utekelezaji wa masharti hayo akiongeza kwamba walishawasilisha
taarifa zote kuhusu maendeleo hayo.
Hivi karibuni Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EUC) na
Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi wa Umoja huo walikutana jijini
Brussels, Ubelgiji kujadili Bajeti ya mwaka 2013 ya umoja huo, ambapo
walitangaza masharti mapya ya utoaji misaada kwa nchi zinazoendelea.
Pamoja na mambo mengine, masharti hayo yanahitaji
uboreshwaji wa haki za binadamu, utawala wa sheria, uwajibikaji katika
matumizi na kudhibiti rushwa.
Akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa
Fedha 2012/2013 bungeni mjini Dodoma Juni mwaka huu, Dk Mgimwa alisema
kuwa katika mwaka huo wa fedha jumla ya Sh15 trilioni zinatarajiwa
kutumika.
Chanzo:- http://www.mwananchi.co.tz
Chanzo:- http://www.mwananchi.co.tz
Post a Comment