HUYU NDIO SANDRA, KOCHA MWANAMKE ANAYEFUNDISHA TIMU YA WANAUME LIGI KUU DRC

Kocha mwanamke, Sandra Makombele wa hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), anayeifundisha timu ya Ligi Kuu ya hapa, Real de Kinshasa leo alikuwa kivutio kikubwa wakati akiiongoza timu hiyo katika mchezo dhidi ya Azam FC Uwanja wa Martyrs, mjini hapa. Nilipozungumza naye, Sandra alisema amesomea ukocha wa soka Cuba kwa miaka saba na zaidi ya Real de Kinshasa alisema anafundisha pia timu ya taifa ya wanawake ya DRC. Lakini alisema anafurahi kufundisha wanaume kuliko wanawake, kwa sababu ya nidhamu. “Wanawake wana dharau sana, lakini wanaume wana heshima, napenda sana kufundisha wanaume,”alisema alipoulizwa kuhusu changamoto anazokutana nazo katika kazi yake.

Sandra kazini

Sandra akibangua bongo zake wakati wa mchezo

Akiwa na kikosi cha Real de Kinshasa leo kabla ya mechi na Azam

Akiwafundisha vijaa wake namna ya kukokota mpira

Sandra kazini

Sandra anamlihsa maarifa kijana wake
Kwa hisani ya:- Bin Zubeiry blog
Sandra anawaandaa vijana kwa mechi

Post a Comment

Previous Post Next Post