MADRID, Hispania
Hatimaye kocha Jose
Mourinho wa Real Madrid amerusha taulo na kusema kuwa timu yake haiwezi
tena kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na
kutetea taji lao msimu huu.
Mourinho amekubali yaishe baada ya
timu yake kushikiliwa kwa sare isiyotarajiwa ya 2-2 kwenye uwanja wao wa
Santiago Bernabeu jana huku mahasimu wao Barcelona ambao wako kilelelni
mwa ligi hiyo wakiibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Atletico
Madrid.
"Sijawahi kuwa katika nafasi kama hii, kupoteza pointi
kibao. Tutajaribu kumaliza msimu vizuri kadri tutakavyoweza. Tutapigania
mataji lakini la ligi kuu linaonekana kwetu kuwa haliwezekani," amesema
Mourinho.
Matokeo ya mechi za jana zilizokuwa za raundi ya 16 yameifanya Real Madrid iachwe na vinara Barcelona kwa tofauti ya pointi 13.

Post a Comment