Kamati ya maandalizi ya Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer of the Year),
imeamua kusogezwa mbele kwa fainali hizo ambazo zilikuwa zifanyike
Desemba 30 mwaka 2012 jijini Dar es Salaam ambapo sasa zitafanyika
Januari 31 mwaka 2013.
Licha ya
hatua muhimu kukamilika lakini zipo sababu za msingi ambazo kamati
imeona ni busara kuzifuatilia ili kufanya tuzo hizo kufanyika kwa
ufanisi.
1. Asilimia
90 (90%) ya Wajumbe wa kamati hiyo ni wanachama wa chama cha makocha wa
Tanzania (Tafca) ambao wapo kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa chama
chao hivyo kushindwa kukamilisha baadhi ya mambo kwa wakati.
2. Pia wapi
baadhi ya wageni muhimu ambao walialikwa asilimia (80%) wameonyesha
kutokuwepo kwa tarehe hiyo (Demsemba 30, 2012) kwa sababu watakuwa nje
ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka jambo
ambalo kamati imeona pia ni jambo la msingi.
Kwa
kuzingatia uzito wa jambo lenyewe kamati imeona ni busara kusogeza mbele
kwa siku 30 kwa lengo la kuwapa nafasi wahusika kwa pande zote mbili
kuendelea na matayarisho hayo ili kuwa na ufanisi kwenye jambo hili la
kitaifa lenye nia ya kusaidia kuinua na kuendeleza vipaji vya soka kwa
Watanzania.
Majina yalioingia fainali
Januari
Mosi 2013, Kamati ya maandalizi ya tuzo za Wazalendo, inarajia
kutangaza majina ya wanasoka ambao wameingia kwenye fainali mwaka 2012.
Hatua hii ni baada ya kukamilisha mchujo wa uliokuwa umefanika hapo
awali wa kupitia majina zaidi ya 93 yaliyopigiwa kura na mashabiki
tangu Agosti-Novemba mwaka huu.
Imetolewa na:-
Ahadi Kakore- Mratibu.

Post a Comment