
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akizungumza katika mkutano na
viongozi wa chama hicho wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Kulia ni Afisa Sera na Utafiti wa chama hicho, Waitara Mwikwabe na
Mwenyekiti wa Jimbo hilo Deogratias Mush. Picha na Michael Jamson
Na n Ibrahim Yamola
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeeo( Chadema), Dk Willbrod Slaa
jana alizungumzia kukatishwa kwake tamaa na mahudhurio ya wajumbe wa
mkutano mkuu wa chama hicho Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Dk Slaa alisema hayo jana wakati wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya mahudhurio kuwa hafifu.
Alisema
asilimia 50 ya mahudhurio ya wajumbe katika jimbo hilo ni aibu na
yanatia shaka iwapo wana nia ya dhati ya kushika dola mwaka 2015.
“Dalili
hii inaonyesha kwamba kuna tatizo, hivyo kupitia mkutano huu
tutayamaliza na kurudisha ufanisi wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Chadema
ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii
itaendelea ya wajumbe kutafutana kwa njia ya simu itakuwa hatari wakati
wa kuunda baraza la mawaziri” alisema na kuongeza:
“Haiwezekani
Rais akawa anatafuta baraza la mawaziri kwa njia ya simu, kwani bila
kujipanga wakati huu itakuwa ngumu huko mbele tunakokwenda,” alisema.
Katika
mazungumzo yake Dk Slaa alisema, wanakusudia kutoa tamko la nini
ifanyike kuhusu mauaji mbalimbali ya wananchi yalifanywa na polisi baada
ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwachukulia hatua Waziri wa Mambo ya
Ndani , Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema
na Kamanda wa Mkoa wa Iringa Michael Kamhanda.
“Hatuwezi
kutulia huku tukiona vyombo ambavyo vinatakiwa kulinda usalama wa raia
ndio vinakuwa vya kwanza kuwaua raia wasiokuwa na hatia huku kiongozi wa
nchini (Rais Kikwete) akiwa kimya bila kutoa tamko lolote,” alisema.
Katika
mkutano huo, wajumbe walitakiwa kufika mapema kwa ajili ya kuanza kwa
mkutano saa 4 hadi saa 6 mchana, lakini kutokana na ufinyu wa
mahudhurio, mkutano huo ulianza saa 6.47 mchana.
Sifa
zimwendee Mwenyekiti wa Chama hicho Jimbo la Kinondoni, Deo Mushi ambaye
alifanya kazi ya kuwatafuta wajumbe hao kwa njia ya simu ili kutimiza
idadi ya asilimia 50.
Mratibu
wa Mkutano huo, Mkurungenzi wa Sera na Utafiti wa Chama hicho, Chacha
Mwita, alisema wajumbe waliokuwa wamefika walikuwa hawana uwezo wa
kuruhusu kufanyika kwa mkutano huo.
Mwita alisema idadi ambayo inatakiwa ya wajumbe wote ni zaidi ya 120, lakini waliokuwa wamefika walikuwa hawazidi 50.
Post a Comment