
Moracka kushoto akiwa na M. Kadinda
Ni kitambo sasa mkali wa 'Crank' Bongo, Mohamed Hassan Mo Racka
amekuwa kimya jambo ambalo limekuwa likizusha nong'ono za hapa na pale
kuwa huenda nyota huyo kafulia kimuziki.
Kupitia mchomvuink pekee stori iliyopo ni kuwa Mo anataraajia kukusanya
mamilioni ya mkwanja kupitia matangazo ya kampuni moja kubwa hapa
nchini dili ambayo kwa asilimia kuwa ndiyo ilimfanya kushindwa kufanya
jambo lolote kwenye gemu ya Bongo fleva.
"Nitakupigia baada ya siku mbili uje kucheki mkataba wa mamilioni ambao
ninatarajia kuusaini na kampuni moja kwa ajili ya matangazo, hilo ndiyo
jambo lililokuwa linanifanya kuwa bize, nafikiri bada ya hapo nitakuwa
poa kufanya kazi zangu za muziki kama kawaida" alisema Mo
Post a Comment