TFF YAMLILIA AMINA SINGO



Amina Singo enzi za uhai wake


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha redio cha 100.5 Times FM, Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia jana.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameongea  leo kwamba msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.
“Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.  TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito,”alisema Wambura.
Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina

Post a Comment

Previous Post Next Post