Zuku Yaingia Mkataba Na Kampuni Ya Max Malipo

Msimamizi Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Max Malipo Bw, Ahmed Lusasi akionyesha Mashine ya kielektroniki Mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya Kuingia mkataba wa Kibiashara na Kampuni ya Zuku  leo katika Hoteli ya Blue Pearl  jijini Dar es Salaam juu ya Kampuni yao kuingia mkataba wa Kuuza Vocha za Zuku  ambapo leo wameweza kusaini Mkataba  utakaowawezesha wateja wa Zuku kulipia Vifurushi vyao popote kupitia mawakala wa Max Malipo.
 
Meneja Mkazi wa Zuku Tanzania Bw, Fadhil Mwasyeba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kuweka  saini mkataba kati ya Zuku na Max Malipo ambapo amesema kuwa wateja wa Zuku nchi nzima watazifurahia huduma zao kwani Max Malipo wanatoa huduma zao nchi nzima ambapo amesema kuwa wameamua kuchukua uamuzi wa kuwashirikisha Max malipo kwani wanatambua ubora wa kazi zao.wakwanza kushoto meneja masoko msaidizi Zuku Bi:Veneranda Raphael.mwisho kulia.Afisa mahusiano na huduma kwa wateja Bi:Mwahamisi Hamisi.
 
Baadhi ya Waandishi waliokuwemo kwenye hafla hiyo
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE

Post a Comment

Previous Post Next Post