![]() |
Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini akiwa amemkunja shati Mshambuliaji wake Mario Balotelli
|
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia ambaye anakipiga katika Klabu ya
Manchester City Mario Balotelli ameendeleza utukutu wake baada ya kutaka
kupiga na Kocha wake Roberto Mancini kwenye Uwanja wa Mazoezi.
Balotelli na Mancini walitaka kupigana kavu kavu kutokana na Kocha huyo
kukwera na namna ambavyo alimchezea vibaya mchezaji mwenzake Scott
Sinclair kwenye mazoezi ya kawaida wa timu hiyo.
Picha zilizopigwa kwenye tukio hilo zinaonesha namna ambavyo Mancini
alivyomvaa mwilini Balotelli ambaye naye hakuonekana kuwa mpole kwenye
tukio hilo ambalo linaongeza wasiwasi wa yeye kuwepo kwenye kikosi cha
Manchester City.
Makocha Wasaidizi wa Manchester City ndiyo ambao waliingilia kati na
kuwatenganisha Balotelli na Mancini huko Kocha huyo akionekana amefura
kwa hasira kutokana na tabia mbaya ya Mshambulizji wake huyo kipenzi.
Makocha wengi wanejikuta wakitamka pasi na ubishi kwa tabia ambayo
inaoneshwa na Balotelli huenda akawa na mwisho mbaya kwenye soka licha
ya kuwa mchezaji kinda mwenye kipaji cha hali ya juu katika kusaka
kabumbu.
Hii ni mara nyingine tena kwa Balotelli kutawala vichwa vya habari kwa
ukorofi wake kwenye mazoezi ya Manchester City kwani hapo awali
ameshazichapa na wachezaji wenzake akiwemo Kollo Toure.
Balotelli mchezaji mwenye vituko vya mara kwa mara na ukorofi
uliopindukia amekuwa akijiona kama mchezaji ambaye anaandamwa zaidi
kutokana na tabia yake kuwakera wengi na amekuwa kaidi kubadilika.
Kocha Mkuu wa Manchester City Mancini anatarajiwa kutoa ukweli wa suala
hilo pale ambapo atakuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baadaye
hii leo akieleza mchezo wao wa Kombe la FA.

Post a Comment