ELTON JOHN NA MUMEWE WAPATA MTOTO WA PILI

Ni mtoto mwingine wa kiume kwa wanandoa Elton John na David Furnish!
Wapenzi hao wa muda mrefu walimpokea mtoto wao wa pili pamoja aitwaye Elijah Joseph Daniel Furnish-John, siku ya ijumaa jijini Los Angeles, kwa mujibu wa jarida la Hello la Uingereza.
Elijah alizaliwa kwa njia ya kitaalam iitwayo ‘Surrogacy’ – ambapo mwanamke hubeba mimba na kuzaa mtoto wa wanandoa ama mtu mwingine.Tayari wapenzi hao wana mtoto mwingine aitwaye Zachary Jackson Levon Furnish-John aliyezaliwa Dec. 25, 2010.

Post a Comment

Previous Post Next Post