HII NDO VIDEO YA OFISA WA TRA ARUSHA ALIYENASWA AKICHUKUA RUSHWA WAZIWAZI....


Video hii imerekodiwa kutoka kwenye simu ya mkononi na inamuonyesha Ofisa wa TRA Arusha akipokea rushwa toka kwa mteja ili aweze kumhudumia. 


Ofisa huyu yupo mapokezi (reception) na inadaiwa ni kawaida yake kupokea Rushwa na kuwa usipompa anadai kwa nguvu.


Wafanyakazi wa TRA na wakubwa zake inadaiwa wanajua kinachoendelea lakini hawachukui hatua.


Kuna utendaji mbovu, lugha chafu kwa wateja na za majivuno na mambo mengi yanayofanana na hayo.


Mamlaka husika zinaombwa kuingilia kati TRA Mapato, (karibu na Benki Kuu tawi la Arusha) ili raia wapate huduma bila vikwazo vya rushwa toka kwa maofisa kama huyu.


Post a Comment

Previous Post Next Post