Jumuiya hii ya siri inapinga dini za kawaida kama Ukristo kwa mujibu wa kitabu cha Simplified Encyclopedia kilichoandika na kuchapishwa na Baraza la Vijana la Waislam Duniani (World Assembly of Muslim Youth) Saudi Arabia na kinafafanua kwamba muasisi wa jumuiya hii ni Herdous Aghriba ambaye alikuwa ni mfalme wa Kiroma.
Waanzilishi hao walichagua majina na alama zao ili kueneza hofu na kuwafanya watu kuamini katika habari zisizo sahihi. Rabai Laquiz ameandika: “Umasoni ni ya Kiyahudi kwa mujibu wa historia yake, uongozi wake, mafundisho yake, zana zake za siri na kazi zake za ubunifu ni za Kiyahudi. “Ilikuwa ikiitwa: ‘Uwezo wa siri wenye lengo la kuwaadhibu Wakristo…kuzuia dini yao kuenea.’ Sasa, imechukua jina hili (Umasoni – Freemasonry) kwa kipindi cha karne kadhaa”.
Neno mason lina maana ya mwenye kujenga nyumba. Hivyo Freemasons lina maana ya wajenzi walio huru. Lakini sasa jina hilo lipo mbali na tafsiri hii.
Enzi hizo ndiyo zilikuwa mwanzo wa umoja huu.
Mwaka 1776 baadhi ya Wakristo waliacha dini zao na kuingia upagani baada ya kuvutiwa na jamii hiyo ya siri wakidhani itawasaidia kuimiliki dunia yote kama mahubiri yao yanavyokuwa yakisisitiza.
Hakuna siri kwamba maandishi yanasema azma ya mwanzo ya Umasoni ni kuupiga vita Ukristo kwa nguvu zote popote pale ulipo kwa siri kubwa.
Baadaye, azma zao ziliendelea kuwa ni kupiga vita dini zote, kuirudisha tena Israel na kuitoa Palestina katika ramani ya dunia.
Nembo zao zikaanza kuenezwa kupitia vifaa, nguo na vitu mbalimbali zikiwemo fedha, mikufu, pete makoti ya askari, hasa wenye vyeo vya juu na kadhalika.
Baadaye wakaingilia viongozi wa siasa kama vile Rais wa kwanza wa Marekani, George Washington (picha kubwa) na baadaye viongozi mbalimbali wa mataifa wakaingia katika jumuiya hiyo ya siri kama Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran.
Post a Comment