RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Zurich, Uswis kwa ajili ya
ziara ya kikazi ya siku 3 ambapo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa
Dunia kuhusu Uchumi katika mji wa Davos.
Mara baada ya kuwasili Zurich, Rais ametembelea makao makuu ya ofisi
za shirikisho la soka duniani, FIFA na kupokelewa na Rais wa FIFA Bw.
Joseph S. Blatter.
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kumshukuru Bw. Blatter kwa kuinua
kiwango cha soka barani Afrika na Tanzania kwa ujumla ambapo misaada
mingi ya kifedha na kiufundi imepatikana kwa ajili ya kuendeleza soka
nchini.
Tanzania ni mwanachama wa FIFA kupitia, Chama cha Mpira Tanzania-Tanzania Football Federation (TFF).
Kama shirikisho mama la mpira duniani, FIFA inajukumu la kukuza na
kuendeleza soka duniani kote na hivyo basi kuweka mikakati na programu
kadhaa za kufanikisha malengo yake ambapo inatoa misaada ya kifedha kwa
nchi wanachama kila mwaka ambapo $.250,000 hutolewa kwa ajili ya miradi
kadhaa na zingine $.2,500,00 hutolewa kwa kila mwanachama, Tanzania
ikiwemo.
Mbali na hiyo kila mwanachama wa FIFA anaweza kupata msaada wa
$.400,000 kila baada ya miaka 4, na msaada huu uliongezwa hadi kufikia
$.500 ,000 tangu mwaka 2010 Kwa ajili ya malengo ya muda mrefu wa
kuendeleza na kuinua soka kwa nchi mwanachama.
Tarehe 24 January, Rais Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
mikutano kadhaa inayoendelea mjini Davos kuhusu Sekta za Maji, Kilimo na
Miundombinu, ambapo anatarajiwa kutoa mada zinazohusu sekta hizo.
Post a Comment