
Justin Bieber anadaiwa kuwa na girlfriend mpya ingawa bado haijawa wazi
kivile hasa baada ya kudaiwa kumwagana na aliyekuwa sweetheart wake
bibie Selena Gomez. Msichana anayedaiwa kutafuna penzi na justin Bieber
anaitwa Milyn Jensen mwenye umri wa miaka 22 akiwa ni mwanafunzi wa
chuo. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa justin wameanza kunong'ona na
hata kuandika kwenye page yake katika mitandao ya kijamii ikiwemo
twitter kuwa Milyn anambemenda Bieber mwenye umri wa miaka 18 wakiwa
wamepishana kwa miaka 4, mashabiki pia wamemwambia kuwa msichana huyo ni
mcharuko na hamfai hata kidogo.“Justin WTF, Milyn Jensen isnt good
enough for you,” wrote one fan online.".Inadaiwa pia Milyn ndo
amechangia Selena kumwagwa. Hata hivyo licha ya watu kuanza kumpa onyo
kuhusu demu huyo yeye anaonekana kutojali na inadaiwa anapokutana nae
humfanyia vituko vya kimahaba msichana huyo mwenye asili ya
African-american.








Post a Comment