KESI YA FILAMU YA JINSIA MOJA YAFUTILIWA MBALI UGANDA


MAHAKAMA moja nchini Uganda, imefutilia mbali kesi dhidi ya mwandishi mmoja wa michezo ya tamthilia, David Cecil, ambaye alikuwa akikabiliwa na shtaka la kuonyesha mchezo kuhusu hali ya wapenzi wa jinsia moja, katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Bwana Cecil, alikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa makusudi.
Bwana Cecil ameiambia BBC, kuwa kesi hiyo ilifutiliwa mbali kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi yake.
Mshukiwa huyo alikamatwa mwezi Septemba, kwa kukiuka sheria za hiyo kwa kuonyesha mchezo huo bila kibali wenye maudhui ''The River and the Mountain''
Bunge la nchi hiyo linajadili uwezekano kwa kuimarisha adhabu ya wale watakaopatikana wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Rais wa Uganda akikagua gwaride la kijeshi
Ikiwa angelipatikana na hatia Bwana Cecil, angelihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.
Alipigwa faini ya laki tano pesa za Uganda, sawa na dola mia mbili za Marekani.
Akiongea muda mfupi baada ya kesi dhidi yake kufutiliwa mbali Bwana Cecil alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi huo, licha ya hofu kuwa huenda akafunguliwa mashtaka mengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post