KICHANGA KINGINE CHATUPWA KTK DAMPO ENEO LA M.R - IRINGA,

Wananchi  wa eneo la M.R mjini Iringa  wakitazama mtoto aliyetupwa kwenye Dampo leo(picha na Patrick Tenywa)
Mwili  wa mtoto aliyetupwa huu ukiwa ndani ya dampo (tunaomba radhi kwa  picha  hizi)
Hapa msamaria mwema akiufunua mwili  huo uliotupwa katika dampo ukiwa katika mfuko wa rambo
Askari polisi wakiupatika  mwili  huo katika Taxi kuupeleka chumba cha maiti  Hospitali ya mkoa  wa Iringa
ZIKIWA  zimepita  siku takribani tano  toka kukutwe kwa mwili  wa mtoto mchanga  katika eneo la Semtema jirani na  makazi ya  wanafunzi  wa chuo  kimoja cha dini  mkoani Iringa ,simanzi na majonzi zimeendelea  kutanda katika manispaa ya Iringa baada ya mtoto mwingine kutupwa katika dampo la taka katika  eneo la stendi ya M.R mjini Iringa.

Wakizungumzia  matukio  hayo ya  wanawake  kufanya  vitendo hivyo  vya ukatili  dhidi ya  watoto  wanaowazaa baadhi ya  wanawake mjini Iringa  wamelitaka  jeshi la polisi na jamii nzima  kusaidiana kuendesha misako mikali  dhidi ya  wanawake  wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili  dhidi ya  watoto  wao.

Sarah Sanga mkazi  wa Miyomboni alisema  kuwa  matukio ya  wanawake kutoa mimba na kutoa watoto  yameendelea  kuwa ni tishio katika Manispaa ya Iringa na kuwa iwapo  jeshi la polisi halitafanya uchunguzi  wa  kina na kuwabaini  wanawake  wanaofanya  vitendo hivyo  vya ukatili yawezekana  matukio hayo yakaendelea  kutikisa katika mji  wa Iringa.

Sanga  alisema  kuwa awali mji  wa Iringa  ulikuwa ukiongoza kwa matukio  kasi ya maambukizi ya VVU ila kwa  sasa matukio yanayotishia zaidi ni ya wanawake  kutoogopa janga la UKIMWI na kuendelea  kushika mimba ovyo na baada ya  kubakiza  miezi michache  ya  kuzaa  wamekuwa  wakifanya ukatili kwa kutoa mimba  hiyo.

" Hivi  hawa  wanawake  wanaoshika mimba na kutupa  watoto kwanini  wanafanya mapenzi bila  kinga ...sasa  leo  mimba  wametoa na kutupa mtoto  na kama  wameambukizwa  UKIMWI nao  watautoa na kuutupa ....dawa ni  kulea mimba na kuzaa salama bila kufanya ukatili huu"

Alisema yawezekana  sababu ya  wanawake  hao  kutoa mimba ikawa ni  wanaume  wanawa wapo mimba  hiyo kuonyesha dalili ya  kuikataa na ndio  sababu ya  kukimbilia  kutoa baada ya  kukataliwa ila yawezekana  pia  wanaohusika na utoaji mimba  hiyo ni  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu ambao wamekuwa wakiishi maeneo ya jirani na maiti hizo za  vichanga  vinapokutwa zikiwa  zimetupwa.

Huku Said Ally akishauri  wanawake  kuwafichua wanawake  wenzao ambao  siku  za karibuni  walionekana na mimba na ghafla mimba hizo kutoweka kwani  iwapo  wanawake  watatoa ushirikiano kwa  kuwafichua  wanaofanya  hivyo vitendo  hivyo  vya kinyama vitapungua .

"Ujue  hapa ambapo  mwili  huu  wa mtoto  umeokotwa katika dampo  kuna Grosary kama mbili  zinazozunguka dampo  hili ila pia ni jirani kabisa la eneo la vibanda  vya UVCCM maarufu kama vibanda  vya kitimoto mjini Iringa hivyo waliotupa mtoto huyo ni wanaotumia dampo  hili na uwezekano  wa  kuwakamata  wahusika ni mkubwa zaidi  kwa  kupiga kura za siri "

Akizungumzia juu ya mwili  huo wa mtoto wa kike  uliokutwa katika dampo hilo la M.R wananchi hao  walisema  kuwa mwili wa mtoto  huyo ambae anakadiriwa  kubakiza kama  wiki mbili ama moja  ili azaliwe  inadaiwa  wahusika wa tukio  hilo ni  wenyeji  wa eneo hilo .


Mkuu  wa  wilaya  ya Iringa Dr. Leticia  Warioba aliwataka  mabinti  na  vijana wilayani  hapo  kuepuka  kukimbilia kushika mimba wala  kupeana  mimba  bila kuwa na uhakika  wa ndoa.

Hata  hivyo  alisema  serikali  ya  wilaya  itaendelea kutoa  elimu  zaidi  kwa  vijana  ili  kupunguza  tatizo la watoto  kutupwa katika wilaya ya  Iringa .

Post a Comment

Previous Post Next Post