NAFASI
ya Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa Pwani (COREFA), Hassan Othman ‘Hassanoo’
kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeota mbawa.
Hassanoo
ambaye yupo mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya kudaiwa kuhujumu uchumi na
wizi wa shaba,
aliomba kuwania nafasi hiyo kupitia Kanda namba 11, inayowakilisha Mikoa ya
Morogoro na Pwani, alichukuliwa fomu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Corefa, Masau Bwire.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF, itamuwia vigumu Hassanoo kushiriki
usaili uliopangwa kufanyika Februari 1 hadi 4 kutokana kuwa mahabusu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratius Lyato, akizungumzia hilo, alijibu kwa kifupi na kuwa, lazima
mgombea ahudhurie usaili mwenyewe na si kutuma mwakilishi.
“Sisi tutapeleka barua za kumtaka kila mgombea
afike kwenye usaili, kinyume na hapo kanuni zipo wazi,” alisema.
Post a Comment