Wikiendi hii Mkurugenzi na muasisi
wa kituo cha kulelea watoto yatima,kinachoitwa Malaika Orphanage
Foundation, Rahma Manji(Pichani kushoto) alipokea msaada kutoka kwa
mwambata wa jeshi kutoka nchini Ujerumani, Bw Abel Gunta(Pichani kulia)
ambaye aliguswa na moyo wa mwenyekiti huyo aliyemua kuanzisha kituo cha
kusaidia watoto baada ya yeye mwenyewe kujikuta akilea watoto wengi wa
ndugu zake kwa sababu mbali mbali takriban miaka 1o iliyopita
Abel ambaye aliambatana na mkewe
walitoa vifaa vya zahanati vikiwemo vitanda na madawa ambavyo kwa ujumla
wake, vimegharimu fedha za kitanzania shilingu milioni 10. Hapa Gunta
akimkabidhi Bi Manji msaada wa madawa huku mkewe Nana, ambaye
aliambatana naye akishuhudia
Vaeni watoto...
Gunta pia alikabidhi fulana ambazo
zitatumika kama sare baada ya masomo kwa watoto hao, hapa akishiriki
katika kuwakabidhi watoto wenyewe. Kituo hicho kilichopo Mkuranga, Mkoa
wa Pwani kina watoto 61 wanaoishi hapo huku 48 wakiwa wanasoma za msingi
zilizopo wilayani Mkuranga, saba shule ya Sekondari na waliobaki wakiwa
hawajafikia umri wa kwenda shule
Hii ni picha ya pamoja ya wanakituo
Chuo kinakabiliana na changamoto mbali mbali katika kipindi hiki ambacho
bado hawajakuwa na miradi ya kujiendesha, vitu kama mavazi, chakula,
ada za watoto ambao wanasoma nje ya Kituo, na waalimu wa kujitolea
kuwafundisha watoto masomo ya ziada baada ya saa za masomo. Kufuatia
hilo unakaribishwa kutembelea Kituo na kujionea mwenyewe hali halisi na
kutoa chochote utakachojisikia iwapo utahamasika.namba ambayo unaweza
kupiga pia ili kupata maelekezo zaidi ni +255 655 786 011 Unaweza
kusaidia wanakituo hawa kupitia akaunti ya KBC namba 3300828357
Post a Comment