Mashali atamba kumpiga kwa KO Mkenya

Mashali alipotwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa kumpiga Med Sebyala
BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali ametamba kumpiga kwa KO mpinzania wake, Benard Mackoliech wa Kenya katika pambano lao la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki litakalofanyika Jumamosu ya Januari 12.
Pambano hiulo la raundi 10 la uzani wa kati litachezwa kwenye  ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam, ambapo Mashali atakuwa akitetea taji hilo baada ya kuutwaa mwaka jana kwa kumpiga Mganda, Med Sebyala.
Akizungumza na MICHARAZO, Mashali alisema kutokana na alivyojiandaa kwa makocha wawili tofauti Charles Mhillu 'Spinks' na Khalled Shomary ana hakika ya kumtwanga Mkenya huyo kwa KO kama kawaida yake.
"Kaka nimejiandaa vema na nitaendeleza kuwapiga wapinzani wangu kwa KO, watanzania wasiwe na hofu nitatetea taji langu na kuwapa raha ya mwaka mpya wa 2013," alisema Mashali.
Mratibu wa pambano hilo, Aisha Mbegu, alisema maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vema na kuwahimiza mashabiki wa ngumi kujitiokeza kwa wingi siku ya Jumamosi ili kupata burudani.
Aisha alisema bondia Mackoliech atawasili nchini siku ya Jumanne kwa ajili ya kupima uzito kabla ya kupanda ulingoni.
“Tunatarajia kushuhudia mpambano mkali ukizingatia Mashali ameweka kambi kwa muda mrefu nje ya mkoa, lakini pia Mackoliech ni bondia mahiri ambaye anasaka rekodi ya kwenda kucheza nje ya nchi”, alisema Aisha.
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Onesmo Ngowi, alisema jana kuwa mapambano ya utangulizi yanatarajiwa kuwa manne na mabondia wote tayari wamesaini mikataba na watatangazwa hivi karibuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post