Mwandaaji wa Mashindano ya Marathon ya Kilomita 10 ya 'MeTL New Years
Eve Midnight Race' Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi
kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 ambapo amewashukuru
Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Kwa kudhamini mashindano
kama haya kwa sababu miaka ya nyuma yalikuwa yakikosa udhamini wa
kuaminika na kwa mshangao wa wengi walikua wakijua Mohammed anadhamini
Soka tu lakini hawajui kwamba hachagui na anadhamini michezo yote.
Kutokana
na udhamini wake sasa tumepata mahali pakujenga uwanja wa Riadha kwa
sababu Uwanja wa Taifa sasa umekuwa kama uwanja wa maonyesho wa soka
lakini riadha tunakusudia kujenga Pwani.
Mwandaaji huyo amemshukuru mdhamini wa michezo hiyo na kusema kwamba
wao kama chama watatimiza malengo ya chama hicho kuitangaza Tanzania
Kimataifa katika riadha.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akizungumza na
waandishi wa habari ambapo ameshukuru ubunifu huu wa kuazimisha mkesha
wa mwaka mpya kwa aina tofauti ambapo watu wengi wamezoea kuadhimisha
katika kumbi mbalimbali za burudani lakini sisi tumeadhimisha mwaka mpya
kimichezo zaidi kwa kufanya Marathon ya Kilometa 10 yaliyojulikana
kama MeTL New Years Eve Midnight Race.
Sisi
kama wanamichezo tumekubaliana na wazo hili la kufanya Marathon kama
hii na tumashukuru MeTL GROUP kwa kudhamini kitu kama hichi cha kipekee n
kuwataka washiriki wajitokeze kwa wingi mara nyingine na pia huu usiwe
mwisho bali uwe ni mwanzo wa kuendeleza michezo Tanzania na tunakiomba
chama cha Riadha RT kushirikiana na wadau wa michezo kukuza mchezo wa
riadha Tanzania.

Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiambatana na
viongozi wa chama cha riadha Tanzania RT kuelekea kuzindua rasmi
mashindano ya riadha ya Kilomita 10 yaliyofanya maeneo ya Masaki jijini
Dar na kumalizika katika Polisi Officers Mess.

Washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamejipanga tayari
kuanza mbio za Marathon 2012 katika mkesha wa mwaka Mpya jijini Dar es
Salaam.

On your Mark...........Get Ready.......Paaaa..... Mgeni rasmi Bw.
Anthony Mtaka aliyenyanyua mkono juu kufyatua baruti kuashiria kuanza
rasmi kwa mbio hizo huku washiriki nyuma yake wakijipanga kushindana
vilivyo.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo kwa upande wa Wanaume Bw. Dickson Marwa akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa 29:14:45.

Baadhi
ya washiriki wengine wakimaliza ngwe ya mashindano hayo ya Kilometa 10
yaliyomalizika katika bwalo la polisi Masaki Jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi
kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania L.t.d (MeTL GROUP) Bw.
Cosmas Mtesigwa akichezea ngoma za asili ya kabila la Wagogo sambamba na
Watumbuizaji hao wakati wa mashindano ya riadha ya 'MeTL New Years Eve
Midnight Race' usiku wa mkesha wa Mwaka mpya 2013 yaliyofanyika usiku wa
kuamkia leo Masaki jijini Dar.

Pichani juu na chini washiriki walifanikiwa kumaliza mbio hizo wakijiandikisha.


Joggers
wakiingia katika viwanja vya Police Officers Mess baada ya kumaliza
ngwe yao katika mashindano hayo ya mbio za kilomita 10 yaliyodhaminiwa
na Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL GROUP) katika
mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2013 usiku wa kuamkia leo.

Mmoja
wa washiriki wa mbio hizo Bw. Said Abrahman kutoka Zanzibar akiwa
amezinduka baada kuzimia alipo maliza ngwe hiyo katika viwanja vya
Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.

Meza
Kuu...Mwakilishi kutoka kampuni ya MeTL GROUP Bw. Cosmas Mtesigwa
akiteta jambo na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony
Mtaka kabla ya kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi kwa washindi.

Pichani
juu na Chini ni Baadhi ya washiriki wa Marathon wakicheza kwaito na
kufurahia baada ya kutimia saa 6 kamili na kuuona mwaka Mpya 2013.

Mwandaaji
wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi
kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwa na waratibu
wengine wa shindano hilo wakiratimisha shindano hilo ili kujua kuweza
nani amepata pointi zipi na kuweza kumtangaza mshindi halali.

Pichani
Juu na Chini ni Mgeni rasmi Rais wa Shirikisho la Riadha nchini
Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiongoza washiriki mashindano ya riadha na
wageni waalikwa kupata chakula cha jioni kabla ya kukabidhi zawadi kwa
washindi.


Rais
Mstaafu wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bw. Francis John akitoa nasaha
kwa washirki ambapo amewataka kuongeza juhudi zaidi na kutokata tamaa
kwa kuwa michezo ni Afya na kuwaasa wananchi wengine zaidi kujitokeza
pamoja na wadhamini wengine katika tukio kama hili ili kuupa kipaumbele
mchezo wa Riadha kama ilivyoonyesha mfano na kampuni ya MeTL GROUP.

Mwandaaji
wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi
kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwatolea uvuvi
viongozi wa vyama vya michezo vya sasa kuwacha kula kwenye michezo ya
wanamichezo na kujikita katika kuvumbua vipaji vipya kwa sababu tumekuwa
tukiwaona walewale kila siku kwa kufanya hivyo mtakuwa hamkuzi mchezo
huu.

Mwakilishi
wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Bw. Cosmas
Mtesigwa akizungumza kwa niaba ya Kampuni ambapo imeahidi kuendelea
kushirikiana na wabunifu wa michezo hii na pia kuendelea kushirikiana
nao bega kwa bega mpaka kufikia michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini
Brazil na kuhakikisha wanapata medali na kuipatia sifa nchi yetu kwa
kuwa na wanamichezo bora.

Rais
wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akiwaasa washiriki
na kutoa shukrani za pekee kwa Kampuni ya MeTL GROUP kwa kuelekeza
macho nguvu zao kusapoti mchezo wa riadha ambao umekuwa haupewi
kipaumbele na wadhamini wengine ambao wamekuwa wakitazama mchezo wa
mpira wa miguu na michezo mingineyo.

Mgeni
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili
kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa
kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve
Midnight Race' Bw. Dickson Marwa aliyemaliza katika muda wa dakika
29:14:45 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka
kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas
Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani
ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania
kwa miaka 10 akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha
Tanzania Bw. Francis John.

Mgeni
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili
kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa
kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve
Midnight Race' Bi. Sara Ramadhani aliyemaliza katika muda wa dakika
33:02:31 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka
kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. Bw. Cosmas Mtesigwa na
Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni
mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10
akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw.
Francis John.

Mwakilishi
kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw.
Cosmas Mtesigwa akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 100,000/= kwa
Mshindi wa tatu kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano
hayo Bw. Mathia Jolo aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika
43:16:07 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers
Mess jijini Dar es Salaam

Mgeni
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili
kulia) akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 500,000/= kwa Mshindi
wa pili kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw.
Shukuru Khalfan aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika
38:51:10 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers
Mess jijini Dar es Salaam.

Mgeni
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili
kulia) akikata keki ya kuukaribisha na mwaka 2013 baada ya kukabidhi
zawadi kwa washiriki wa Marathon za Mbio za Kilometa 10 usiku wa kuamkia
leo jijini Dar.

MgeniRais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akifungua
rasmi muziki kwa wote baada ya zoezi la kukabidhi zawadi.

Post a Comment