Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye kijiji cha Mswakini
Wilayani Monduli tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa vikoba katika
kijiji hicho.Katikati ni Mkewe Mama Regina Lowassa aliefatana nae kwenye
hafla hiyo ya Uzinduzi wa Vikoba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa
wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli
walipowasili tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba katika kijiji
hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa
kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli wakati wa hafla ya uzinduzi wa
VIKOBA kijijini hapo.Mh. Lowassa katika hotuba yake,amesema kuwa
ushirika wa VIKOBA ni sawa na mshipa wa damu kwa sera ya maisha bora kwa
kila Mtanzania,pia alisema kuwa kutokana na kutambua hivyo ushirika wa
Vikoba utaanzishwa katika wilaya nzima ya Monduli.Miasha bora kwa kila
Mtanzania ni sera aliyoingia nayo madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya
Monduli,Bi Judith (kulia) akikabidhi kwa Mhe. Edward Lowassa hati
maalumu ya uzinduzi wa Vikoba ili ikabidhiwe kwa Wananchi Mswakini
Monduli.
Baadhi ya wanachama wa Vikoba wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli.
Post a Comment