
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe ameamua kuweka wazi kuhusu kugombea uraisi mwaka 2015, alifunguka kwa kusema,
"Ngoja
niweke wazi kabisa. Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya
kauli za wanachama waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala
hilo. Jibu langu kwa wote wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba
'katika moja ya maazimio yangu ya mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa
suala la Urais 2015. Hivyo sitaongelea suala hili. Sitasema kitu kuhusu
suala hili mpaka baada ya Katiba mpya kupatikana na chama changu kuweka
utaratibu na mchakato wake'.
Post a Comment