MT. KILIMANJARO DAY 2 - 3

Siku ya pili tuliamkia safari ya kutoka MANDARA HUT kuelekea HOROMBO HUT
Safari ilituchukua masaa 9 kwa kutembea kutokana na mwendo wetu
Kwa kawaida wazoefu hutembea masaa 6 tu..ila kwa sisi, tulibonyea.

Kutoka Mandara kwenda Horombo ni Km  11
Usizifikirie km 11 za tambarare ndugu, zifikirie kuwa unazitembea kwa kupanda juu


 KIBO unaiona kwa mbali unadhani ni karibu kufika na unaitamani
Ila ukiianza safari ya kukasogelea kale ka kofia ka barafu utasali Malaika waje wakunyakue wakurushe hapo juu uache kutembea


 Ukipanda juu Horombo Hut (Camp) unaiona kwa chini


Juu kila mtu anaependa kujitengenezea kamlima kake kadogo kama kumbukumbu na kuacha hapo
Why not?? Nilifanya wa kwangu pia
 Mabadiliko ya ngozi yalianzia hapa taratibu

 Mawenzi unaiona kwa nyuma yetu kwenye background??


Kushoto ni Justin Bayor (Cameraman wa Diary, Jide & Captain)

 Baridije sasa?
Meshak (tour guide) wa katikati aikuwa ananisaidia kupuliza pen itoe wino ili iandike alama kwenye kamlima kangu niliko katengeneza juu ya Kilimanjaro
Ilibidi pen tuondoe ile ncha ya mbele ya kuandikia, ndio tupulize wino ili utoke mwingi wa kutosha kuandikia



Baaaasi

Post a Comment

Previous Post Next Post